Thursday, 2 February 2017

Malighafi ya Kutengeneza Mabomu ya Nyukilia: Plutonium-239: Malighafi ya Nyukilia ya Kolonia Santita Sawa na Aliyoiba Martin Turner Smith Kutoka kwa Kiongozi wa Guanajuato kwa Makubaliano na Vyama Haramu vya Msituni vya Kolombia

Plutonium huzalishwa kutokana na matumizi ya mafuta ya uranium katika mitambo ya nyukilia. Hupatikana ndani ya mafuta yaliyotumika ya uranium mara tu baada ya kutolewa ndani ya mtambo, lakini plutonium huweza kuchujwa kwa kuchakatajiwa tena (‘reprocessing’) baada ya mafuta hayo kuhifadhiwa katika hatua za mwanzoni. Kisha plutonium (iliyochujwa kutoka ndani ya mafuta yaliyotumika ya uranium) huweza kutumika tena kama mafuta ya mtambo, au kuhifadhiwa kwa ajili ya maamuzi mengine ya kiutawala. Nchini Uingereza kuna aina nne tofauti za plutonium, zinazotokana na hatua mbalimbali za uchakataji wa plutonium kama ifuatavyo hapa chini.

1 – Plutonium ndani ya mafuta yaliyotumika ya uranium.

2 – Plutonium iliyochujwa kutokana na uchakataji wa mafuta yaliyotumika tena.

3 – Plutonium ndani ya mchanganyiko wa ‘plutonium oxide’ na mafuta ya uranium.

4 – Plutonium ndani ya vitu vilivyoambukizwa wakati mifumo ya uchakataji ikiendelea.

Plutonium-239 ya Kolonia Santita (iliyoibwa na El Padrino kutoka Los Alamos na baadaye kuibwa na Martin Turner Smith kutoka kwa El Padrino) ilikuwa sehemu ya mpango kamambe wa Panthera Tigrisi ambao Tume ya Dunia haikuujua, wa kutawala biashara ya kokeini ya Kolombia – chini ya utawala wa ‘magorila’ wa Amerika ya Kusini.

Nchi zinazonunua mitambo na vinu vya kutengenezea plutonium hujitetea kwamba zinavihitaji kwa ajili ya matumizi salama ya uzalishaji wa umeme. Lakini kwa kuzalisha umeme, mitambo na vinu vya nyukilia si teknolojia ya muhimu sana kiuchumi, hasa katika nchi zinazoendelea za dunia ya tatu. Kwa nchi zenye mitambo na vinu vya kutengenezea plutonium vinu vya plutonium ni miradi ya bure, maana umeme unaweza kuzalishwa kwa njia zingine mbadala. Kwa nini nchi nyingi zisizokuwa na silaha za nyukilia hupendelea sana teknolojia ya nyukilia? Lazima kuwepo na sababu kubwa isiyokuwa ya kiuchumi, ambayo huenda ndiyo hiyo ya kutengeneza silaha za nyukilia, hasa kwa mataifa ya kigaidi na yanayojiona yametengwa na dunia.

Njia pekee ya kupunguza plutonium na hivyo kupunguza matumizi ya kijeshi ya madini hayo ya kikemikali ni kutumia mafuta ya MOX (‘Mixed Oxide’, mchanganyiko wa ‘plutonium oxide’ na mafuta ya uranium) katika mitambo ya nyukilia kwani plutonium huchomeka na kwisha, ingawa si kwisha kabisa – kwa sababu ‘chain reaction’ huzalisha plutonium nyingine mpya, lakini hii ni kwa kiasi kidogo. Makampuni ya kinyukilia yatumie asilimia kubwa zaidi ya MOX kuliko mafuta mengineyo, katika mitambo na vinu vya nyukilia; kama inavyofanya Marekani, Ufaransa, Urusi na Japani.

1 comment:

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...