Biblia
pamoja na historia vinatwambia kuwa mitume kumi na wawili wa Yesu
Kristo waliamua kufa kinyama kama mfalme wao alivyokufa, kwa sababu
walikataa kukana imani yao juu ya Yesu Kristo.
Mathayo
alikufa kwa ajili ya Ukristo nchini Ethiopia kwa jeraha lililotokana na
kisu kikali, Marko akavutwa na farasi katika mitaa ya Alexandria nchini
Misri mpaka akafa, kwa sababu alikataa kukana jina la Yesu Kristo.
Luka alinyongwa nchini Ugiriki kwa sababu ya kuhubiri Injili ya Yesu Kristo katika nchi ambapo watu hawakumtambua Yesu.
Yohana
alichemshwa katika pipa la mafuta ya moto katika kipindi cha mateso
makubwa ya Wakristo nchini Roma, lakini kimiujiza akaponea chupuchupu,
kabla ya kufungwa katika gereza la kisiwa cha Patmo (Ugiriki) ambapo
ndipo alipoandika kitabu cha Ufunuo. Mtume Yohana baadaye aliachiwa huru
na kurudi Uturuki, ambapo alimtumikia Bwana kama Askofu wa Edessa.
Alikufa kwa uzee, akiwa mtume pekee aliyekufa kwa amani.
Petro
alisulubiwa kichwa chini miguu juu katika msalaba wa umbo la X
kulingana na desturi za kikanisa za kipindi hicho, kwa sababu aliwaambia
maadui zake ya kuwa alijisikia vibaya kufa kama alivyokufa mfalme wake
Yesu Kristo.
Yakobo
ndugu yake na Yesu (Yakobo Mkubwa), kiongozi wa kanisa mjini
Yerusalemu, alirushwa kutoka juu ya mnara wa kusini-mashariki mwa hekalu
aliloliongoza la Hekalu Takatifu (zaidi ya futi mia moja kwenda chini)
na baadaye kupigwa kwa virungu mpaka akafa, alipokataa kukana imani yake
juu ya Yesu Kristo.
Yakobo
mwana wa Zebedayo (Yakobo Mdogo) alikuwa mvuvi kabla Yesu Kristo
hajamwita kuwa mchungaji wa injili yake. Kama kiongozi wa kanisa
hatimaye, Yakobo aliuwawa kwa kukatwa kichwa mjini Yerusalemu. Afisa wa
Kirumi aliyemlinda Yakobo alishangaa sana jinsi Yakobo alivyolinda imani
yake siku kesi yake iliposomwa. Baadaye afisa huyo alimsogelea Yakobo
katika eneo la mauti. Nafsi yake ilipomsuta, alijitoa hatiani mbele ya
hakimu kwa kumkubali Yesu Kristo kama kiongozi wa maisha yake; halafu
akapiga magoti pembeni kwa Yakobo, ili na yeye akatwe kichwa kama mfuasi
wa Yesu Kristo.
Bartholomayo,
ambaye pia alijulikana kama Nathanali, alikuwa mmisionari huko Asia.
Alimshuhudia Yesu mfalme wa wafalme katika Uturuki ya leo. Bartholomayo
aliteswa kwa sababu ya mahubiri yake huko Armenia, ambako inasemekana
aliuwawa kwa kuchapwa bakora mbele ya halaiki ya watu iliyomdhihaki.
Andrea
alisulubiwa katika msalaba wa X huko Patras nchini Ugiriki. Baada ya
kuchapwa bakora kinyama na walinzi saba, alifungwa mwili mzima kwenye
msalaba ili ateseke zaidi. Wafuasi wake waliokuwepo katika eneo la tukio
waliripoti ya kuwa, alipokuwa akipelekwa msalabani, Andrea aliusalimia
msalaba huo kwa maneno yafuatayo: “Nimekuwa nikitamani sana na nimekuwa
nikiitegemea sana saa hii ya furaha. Msalaba uliwekwa wakfu na Mwenyezi
Mungu baada ya mwili wa Yesu Kristo kuning’inizwa juu yake.” Aliendelea
kuwahubiria maadui zake kwa siku mbili zaidi, akiwa msalabani, mpaka
akaishiwa na nguvu na kuaga dunia.
Tomaso
alichomwa mkuki nchini India katika mojawapo ya safari zake za
kimisionari akiwa na lengo la kuanzisha kanisa la Yesu Kristo katika
bara la India.
Mathiya
alichaguliwa na mitume kuchukua nafasi ya Yuda Iskarioti, baada ya kifo
cha Yuda katika dimbwi la damu nchini India. Taarifa kuhusiana na
maisha na kifo cha Mathiya zinachanganya na hazijulikani sawasawa.
Lakini ipo imani kwamba Mathiya alipigwa mawe na Wayahudi huko
Yerusalemu, kisha akauwawa kwa kukatwa kichwa.
Yuda Tadei, ndugu yake na Yesu, aliuwawa kwa mishale alipokataa kukana imani yake juu ya Yesu Kristo.
Mitume
walikuwa na imani kubwa kwa sababu walishuhudia ufufuo wa Yesu Kristo,
na miujiza mingine. Biblia ni kiwanda cha imani. Tunapaswa kuiamini
Biblia kama mitume walivyomwamini Yesu Kristo, kwa sababu Biblia
iliandikwa na mitume.
Mitume
kumi na wawili wa Yesu Kristo waliamua kufa kinyama kulinda heshima ya
mfalme wao Yesu Kristo, kama Biblia na historia vinavyosema. Kwa nini
watu (wengine) wa kizazi hiki wanasema hakuna Mungu na kwa sababu hiyo
hawamwamini Yesu? Je, uko tayari kufa kwa ajili ya mtu aliyekufa kwa
ajili yako? Kwa ajili ya mtu ambaye mitume walikuwa tayari kufa kwa
ajili yake? Je, wewe una akili zaidi kuliko mitume? Yesu aliamua kufa
ili wewe uishi, lakini bado unakuwa mbishi. Badilika.
No comments:
Post a Comment