207.
 Mtu akikuita mjinga au mpumbavu juu ya maisha yako usikasirike kwa 
sababu wewe si mjinga wala mpumbavu. Sema hapana kwa ndiyo nyingi kwa 
sababu hawapaswi kuingilia mambo ya mtu mwingine bila idhini ya Mwenyezi
 Mungu. Kuingilia mambo ya mtu mwingine bila idhini ya Mwenyezi Mungu ni
 dhambi, tena dhambi kubwa, ni kuvunja amri kuu ya kwanza ya Mungu. 
Mungu
 ana mpango na maisha ya kila mtu hapa duniani bila kujali dini, jinsia,
 kabila, rangi, taifa, au umri, na kila mtu ni wa kipekee. 
Usiingilie
 mambo ya mtu mwingine bila kibali kutoka kwa Mungu. Kuingilia mambo ya 
mtu mwingine bila kibali kutoka kwa Mungu ni dhambi. Dhambi hiyo 
itakuathiri. Hivyo, jali mambo yako – ya mwingine Mungu anayafanyia kazi
 – hadi utakapoitwa na Mungu kuingilia kati. Kuingilia kati mambo ya mtu
 mwingine kunaweza kuathiri mpango wa Mungu katika maisha yake. Hivyo, 
acha. 
Kama
 John Doe ana matatizo katika maisha yake acha ayatatue mwenyewe. 
Akishindwa atakuomba ushauri au ataomba ushauri kutoka kanisani kama ni 
Mkristo, au msikitini kama Mwislamu, au kutoka katika nyumba yoyote ya 
ibada kulingana na imani yake. Mtu akikuomba ushauri mshauri kwa moyo 
wako wote, wala usimshauri kwa unafiki au kinyongo cha aina yoyote ile. 
Wewe
 kuingilia mambo ya John ni sawa na kusema, “Mungu umeshindwa hebu ngoja
 na mimi nijaribu; ngoja niingilie kati kukusaidia juu ya maisha ya John
 Doe.” Hiyo ni dhambi. Tena ni dhambi kubwa. Unajifananisha na Mungu; 
kwamba Mungu wa John Doe ameshindwa kwa hiyo mungu wewe ndiye 
utakayemtatulia matatizo yake. Amri kuu ya kwanza ya Mungu inasema, 
“Usiwe na miungu mingine ila mimi.” Kuingilia mambo ya John tayari 
umevunja amri ya kwanza ya Mungu kwa kujifanya Mungu. Mungu ana mpango 
na maisha ya John, na anatumia matatizo yake kumfikisha kwenye takdiri 
aliyompangia. Hivyo, wewe si Mungu, acha Mungu afanye kazi yake. Mungu 
akikuruhusu kuingilia kati, yaani John akiamua kwa hiari yake mwenyewe 
kukuomba msaada wa mawazo au ushauri, maana yake ni kwamba Mungu 
amekuchagua wewe kuwa sehemu ya mafanikio ya John Doe. 
John Doe ni jina la mtu mwanamume asiyekuwa na jina. Mwanamke anaitwa Jane Doe. 

Historia ya maisha yangu ni yangu. Wewe ni nani kusema historia yangu si ya kweli?
ReplyDeleteUmesikia mtaani kwamba mke wa kaka yako anatembea na teja, na ukathibitisha, lakini bila kaka yako au shemeji yako kujua. Je, utamwambia kaka yako? Je, utamwambia shemeji yako? Je, utawambia watu wengine? Jibu unalo.
ReplyDelete