Bastola
ya kalamu ya John Murphy Ambilikile aina ya Stinger; iliyotumiwa na
Murphy kumuua kinyama jambazi sugu wa CS-Moscow – Tawi la Kolonia
Santita nchini Urusi na nchi zote za Ulaya ya Mashariki; na baadhi ya
nchi za Ulaya ya Kusini kama vile Masedonia, Montenegro, Uturuki na
Ugiriki – Vladimir, huko Yugo Zapadnaya mjini Moscow, katika ‘dacha’ ya
Kolonia Santita.
Bastola
ya kalamu aina ya Stinger (tamka ‘Sting’a’) ni silaha ‘halali’ kwa
matumizi ya kawaida ya binadamu huko nchini Marekani hadi hii leo;
halali kwa maana ya ATF – shirika la pombe, tumbaku na silaha la
Marekani – kuichukulia kama silaha ya kawaida. Lakini Stinger ya John
Murphy haikuwa (wala haijawahi kuwa) silaha ya kawaida! Ilitengenezwa
kwa ajili ya matumizi ya Idara ya Usalama ya Tume ya Dunia (WIS – ‘WODEC
Intelligence Services’) na kwa ajili ya matumizi ya Kikosi cha
Kikomandoo cha Tume ya Dunia (EAC – ‘Executive Action Corps’).
Stinger
ya Murphy ilikuwa na uwezo wa kubeba risasi moja ndogo kwa wakati mmoja
– iliyokuwa na ukubwa wa inchi 0.22 ya mtutu wa bunduki (‘.22 caliber’)
– na kidonge kimoja cha ‘cyanide’ (‘potassium suicide pill’): ili
akitekwa akimeze na kufa; kuliko kutoboa siri za EAC, na siri za Tume ya
Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya.
Aidha,
Stinger ya Murphy ilikuwa na uwezo wa kufyatua risasi ikiwa imenyooka
(Stinger ya kawaida hufyatua risasi ikiwa imejikunja) na kifyatulio
chake kilikuwa kwenye kichwa cha kalamu; na ilikuwa na koki mbili: moja
kwa ajili ya risasi, na nyingine kwa ajili ya mrija wa kalamu, tofauti
na Stinger ya kawaida ambayo ina koki moja, mbele ya kifyatulio. Stinger
ya Murphy ilikuwa na uwezo wa kuandika kama kalamu ya kawaida! Ilikuwa
na uwezo wa kutumia kiwambo cha kupunguza sauti, kama Stinger za
kawaida.
Kalamu ya John Murphy
ReplyDelete