Desierto de Los Leones au Jangwa la Simba kwa Kiswahili, mgahawa wa
watu wakubwa wa Latino, kusini-magharibi mwa Mexico City, katika
Kitongoji cha San Ángel, katika Wilaya ya Álvaro Obregón, John Murphy na
Frederik Mogens walipokutana na watoto wa wakubwa wa Meksiko Debbie
Patrocinio na Lisa Graciano, katika mazingira ya usalama wa hali ya juu
wa WODEC Intelligence Services WIS na PSD ambacho ni kikosi maalumu cha
ulinzi wa rais wa Meksiko.
Sifa kubwa ya Murphy ni udadisi, lakini
kubwa zaidi ni unyamaume. Haogopi kitu. Anaheshimu sheria. Jumatano saa
nne asubuhi, Murphy na Mogens walikutana na Debbie Patrocinio Abrego
(na rafiki yake mpenzi Lisa Madrazo Graciano) katika Baa ya Desierto de
Los Leones, San Ángel, kusini-magharibi mwa Mexico City. Miadi kama hiyo
John Murphy huwa haichukulii mzaha hata kidogo! Ndani na nje ya baa:
Radia, Yehuda na maafisa wengi wa WODEC-Intelligence walitapakaa kila
mahali; kumlinda Murphy na Sajini Mogens. Murphy na Morgens walifurahi
kumwona Debbie (kwa mara nyingine) na walikuwa na hamu ya kumjua vizuri
yeye na rafiki yake. Muda ulizidi kwenda. Kengele ya hatari ndani ya
kichwa cha Murphy ilizidi kulia. Mogens alianza kubadilika! Naam.
Kutetea afya na amani ya dunia, Operation Devil Cross ilianza kazi
rasmi! Kilichotokea baada ya hapo kilibadilisha historia ya Tume ya
Dunia milele.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Roho Yako
289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...
-
KITENDAWILI CHA KOLONIA SANTITA Shilingi milioni moja za Kitanzania kushindaniwa ndani ya miezi sita kuanzia leo Swali: Kila namba ...
-
Mpelelezi wa Tume ya Dunia kutoka Jerusalem, Israeli, Kanali Daniel ‘Yehuda Ben-Asher’ Ebenezer, Daniel Yehuda, alikuwa komandoo wa kit...
-
Uwanja wa Ndege wa Copenhagen-Roskilde: uliotumiwa na Tume ya Dunia na Kolonia Santita kwa pamoja – kilometa tisa kutoka katika Kanisa ...

No comments:
Post a Comment