Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Guadalajara, Jalisco, Meksiko. Ndege ya Vijana
wa Tume, Grumman Gulfstream IV, ilitua katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Guadalajara saa saba usiku CST kutokea Copenhagen; Vijana
wa Tume wakaingia Mexico City saa kumi alfajiri CST, katika mazingira ya
kutatanisha.
Kamanda
wa Jeshi la Polisi la Tume ya Dunia Kanda ya Amerika ya Kaskazini Meja
Jenerali Sebastian Alejandro, na maafisa sita wa WODEC-Intelligence
kutoka Mexico City, alikuwepo na wenzake katika Uwanja wa Ndege wa
Guadalajara huko Jalisco kuwapokea Vijana wa Tume, kwa amri ya Jeshi la
Anga la Meksiko ('Fuerza Aérea Mexicana') na Idara ya Usalama ya Tume ya
Dunia, alipewa jukumu la kuwaingiza Vijana wa Tume jijini Mexico City
kwa magari ya SUV na 'ambulance' kama wagonjwa mahututi. Katika nyumba
yao ya siri waliyopewa na Jeshi la Anga la Meksiko, Calle Gante,
Cuauhtémoc (tamka 'Kwauteimak'), katikati ya Mexico City, Vijana wa Tume
walipata ugeni wa ghafla kama walivyoelezwa na Mkurugenzi wa Usalama wa
Tume ya Dunia Christoffer Sortevik huko Copenhagen. Mmoja wa wageni hao
(Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Meksiko (PGR) Virgilio Santo
Graciano, Mkuu wa Jeshi la Polisi Meksiko (PJF) Demetrio Vega del
Castilo, Kiongozi wa Kanda ya Amerika ya Kaskazini ya Tume ya Dunia
Kamishna Profesa Randall Buchanan Ortega wa Marekani, Mkuu wa Mamlaka ya
Kudhibiti Madawa ya Kulevya Marekani (DEA) Baxter Salvatore Sincere, na
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu (CNDH) Daktari Santiago
Luis-Fernando) alikuwa kibaraka wa Kolonia Santita, ingawa alikuwa
kibaraka wa Kolonia Santita kwa shingo upande.
Wageni
hao (viongozi wakubwa katika vita dhidi ya madawa ya kulevya duniani)
walikwenda kuwajulia hali Vijana wa Tume na kuwapa hali halisi ya
usalama ya Mexico City na ya Kateli ya Kolonia Santita; lakini miadi ya
Vijana wa Tume na Debbie na Lisa (mtoto wa rais na mtoto wa naibu
mwanasheria mkuu wa Meksiko kwa mpangilio huo) kesho yake katika Baa ya
Desierto de Los Leones huko San Ángel, ilibadili kabisa historia ya
Kolonia Santita na ya Tume ya Dunia.
No comments:
Post a Comment