Friday, 2 December 2016

Uwanja wa Ndege wa Copenhagen-Roskilde

Uwanja wa Ndege wa Copenhagen-Roskilde: uliotumiwa na Tume ya Dunia na Kolonia Santita kwa pamoja – kilometa tisa kutoka katika Kanisa la Roskilde, sawa na Kanisa la Westminster Abbey la London, katika makaburi ya wafalme na Wadenishi maarufu.

Uwanja wa Ndege wa Roskilde: ulitumiwa na ndege za Kolonia Santita na Tume ya Dunia kwa wakati mmoja (Gulfstream Grumman) kuingia na kutoka katika jiji la Copenhagen. Baada ya kubomoa kambi za Kolonia Santita za Saltholm na Smallegade za Copenhagen kwa usiku mmoja, Vijana wa Tume waliondoka wote kupitia Roskilde kuelekea Meksiko. Huko walitakiwa kusimamisha usafirishaji wa tani 600 za madawa ya kulevya na kilo 1 ya malighafi ya nyukilia, kubomoa meli na nyambizi za Kolonia Santita, kubomoa majengo, kubomoa silaha, kupeleleza kujua HVT (Panthera Tigrisi) ni nani, kupeleleza kujua historia ya HVT, kupeleleza kujua lengo la HVT, na kumbomoa adui na majeshi yake yote. Hapo kuna taharuki (‘cliffhanger’) kubwa kuliko zote katika kitabu cha Kolonia Santita.

HVT (‘High Valued Target’) au STKJ (Shabaha ya Tume ya Kiwango cha Juu) ni mtu muhimu zaidi anayetafutwa na Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya. Katika kitabu cha Kolonia Santita mtu huyo ni Panthera Tigrisi; anayejulikana pia kama El Tigre, The Tiger, Jefe de Jefes, Bosi wa Mabosi, Chui wa Siberia, miongoni mwa majina mengi, ambayo yote ni ya bandia. Kumkamata Bosi wa Mabosi haiwezi kuwa kazi rahisi. Ndiyo maana tume ikaandaa Vijana wa Tume kutoka Executive Action Corps, kitengo maalumu aula cha makachero-wanajeshi-makomandoo cha Tume ya Dunia, ambacho ni bora kuliko mashirika mengi ya kijasusi duniani.

No comments:

Post a Comment

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...