Tuesday, 6 December 2016

Mimi

Mimi ni mwana wa Mungu. Sisi sote ni watoto wa Mungu. Lengo la kuzaliwa kwangu ni kufanya kazi pamoja na Roho Mtakatifu na malaika kumtumikia Bwana, na kueneza injili ya Yesu Kristo duniani kote, kupitia vitabu.

Nilijifunza toka awali umuhimu wa kushindwa katika maisha ijapokuwa nilijitahidi sana, na nilipoendelea kushindwa niliweka nadhiri ya kufanya kitu kimoja kilicholeta maana zaidi katika maisha yangu nacho ni uandishi wa vitabu. Uandishi wa vitabu ndicho kitu pekee nilichokiweza zaidi kuliko vingine vyote na kuanzia hapo Mungu aliniweka huru. Nilijua mimi ni nani. Nilijua kwa nini nilizaliwa. Nilijifunza falsafa ya kuacha dunia katika hali nzuri kuliko nilivyoikuta – kwa sababu hata mimi nilikuwepo – na falsafa ya kushindwa si hiari. Maarifa hayo yakafanya niwe na heshima na upendo kwa watu wote.

1 comment:

  1. Kama si kwa ubatizo basi sisi ni watoto wa Mungu kwa uumbaji – kama inavyoonyeshwa katika vitabu vya Mwanzo, Wagalatia, Ezekieli, na Matendo ya Mitume.

    “Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.” (Mwanzo 1:26-27).

    “Tazama, roho zote ni mali yangu; kama vile roho ya baba ni mali yangu, ndivyo ilivyo roho ya mwana mali yangu; roho ile itendayo dhambi itakufa.” (Ezekieli 18:4).

    “Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Yesu Kristo. Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo.” (Wagalatia 3:26-27).

    “Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. Kama vile mmoja wenu, mtunga mashairi alivyosema, , Maana sisi wote tu wazao wake.” (Matendo 17:28).

    Yehova ‘humiliki’ kila mtu hapa duniani, na anaweza kutubariki au kutuadhibu kutegemeana na jinsi tunavyolipokea neno lake.

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...