202.
Matatizo ya kijamii, kimiiko, kimaadili, kisiasa, na kiroho; hayataweza
kutatuliwa kwa pesa, vikao vya kifamilia, haki za binadamu, usalama wa
taifa, au nguvu za kijeshi. Yataweza kutatuliwa kwa haki na hekima ya
Mwenyezi Mungu.
Israeli
ilifikia kikomo cha kipindi chake kikubwa cha mafanikio tangu enzi za
Sulemani. Taifa lilikuwa tajiri. Lilikuwa na nguvu. Lilikuwa na silaha
nyingi na nzuri zaidi. Lilikuwa taifa lililojidai kwa uwezo wake mkubwa
wa nguvu za kijeshi, hekima, ujasiri, utajiri, na faida za kimkakati.
Nani angeweza kushindana na Israeli? Lakini Mungu hunguruma onyo kwamba
uwezo wote mkubwa wa asili wa taifa, ujuzi waliojipatia, na sifa bora
zaidi havikuweza kulisaidia taifa la Israeli. Watu huona nguvu ya taifa
katika utajiri wake, idadi yake ya watu, silaha za kijeshi, teknolojia,
na maarifa. Lakini Mungu huangalia haki.
Kwa
vile taifa la Israeli lilipoteza haki yake ya upendeleo, Mungu aliahidi
kuliharibu kama alivyoyaharibu mataifa ya Waamori na Wamisri. Watu wa
Israeli walishafika mbali sana kiasi cha Mungu kutokutegemea tena toba
kutoka kwao. Kuna muda wa fursa na kuna muda ambao fursa haipo tena.
Nafasi ya Israeli ya kutubu ilishafikia mwisho.
Kama
alivyokuwa amepigana vita vyao kwa ajili yao katika siku za nyuma sasa
Mungu alipigana nao. Pamoja na ujasiri na utaalamu wao wote
wasingependelewa tena. Mambo ambayo mwanzo yaliipa Israeli nguvu katika
vita yaliwageukia.
Israeli,
kama adhabu kwa uozo wake wa kiroho na kimaadili, ilivamiwa na Ashuru
katika mwaka wa 721 BC na kuangushwa vibaya katika vita hiyo kubwa.
Waisraeli waliosalia walitekwa na kupelekwa uhamishoni ambako inaonekana
walitoweka kabisa katika uso wa dunia hii. Hili lilikuwa ni jibu la
Mungu kwa dhambi na uasi wao.
Sababu
ya kupanda na kuanguka kwa mataifa ni ya kimaadili na kiroho. Hakuna
taifa linaloweza kutegemea nguvu na mali zake ili kujiokoa kutokana na
madhara ya ukiukwaji wa maadili.
Dhambi ikizidi katika taifa, Mungu ataliangamiza. Taifa likitenda haki, Mungu ataliinua.
Uovu ni aibu kwa taifa zima!
ReplyDelete