Kikamilikacho si kiimarishwacho. Rais wa Tume ya Dunia alilazimishwa,
 kufanya kazi aliyokuwa amejitolea maisha yake yote kuipigania kwa nguvu
 zake zote, na utendaji wake mzuri wa kazi uliharibika.
Kitu 
kikishakamilika hakiwezi tena kuimarishwa ukilazimisha utakiharibu. Rais
 wa Tume ya Dunia, Boidin Tony Versnick, alitishwa na Umoja wa Mataifa 
kuondolewa katika wadhifa wake iwapo angeshindwa kumkamata Panthera 
Tigrisi ndani ya siku saba bila kujali uaminifu, uthabiti, uvumilivu,
 uadilifu na uchapakazi wake hodari katika Tume ya Dunia. Mbali na 
ukamilifu huo katika kazi hata hivyo, kilichokamilika kililazimika 
kuimarishwa. Versnick ndani ya hizo siku saba alipigana kufa na kupona 
kutetea wadhifa wake, thamani yake ya utu na kujitengenezea nafasi nzuri
 katika historia ya Tume ya Dunia na ya Umoja wa Mataifa na ya dunia kwa
 jumla. Hakuzijali tena sifa zake za kazi, hakujali sheria, hakujali 
vitisho vya Umoja wa Mataifa. Lakini pamoja na kazi nzuri aliyofanya, 
Boidin Versnick alilazimika kujiuzuru wadhifa wake; nafasi yake 
ikachukuliwa na Makamu wa Rais wa Tume ya Dunia, Jørgen Vestergaard 
Laursen, aliyekuwa na umri wa miaka sitini na mchapakazi hodari kutoka 
Denmaki. Versnick alipigana na Kolonia Santita kwa pupa, licha ya 
shinikizo la Umoja wa Mataifa. Usimlazimishe mtu kufanya kazi ambayo 
tayari anaifanya vizuri.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Roho Yako
289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...
- 
KITENDAWILI CHA KOLONIA SANTITA Shilingi milioni moja za Kitanzania kushindaniwa ndani ya miezi sita kuanzia leo Swali: Kila namba ...
 - 
Mpelelezi wa Tume ya Dunia kutoka Jerusalem, Israeli, Kanali Daniel ‘Yehuda Ben-Asher’ Ebenezer, Daniel Yehuda, alikuwa komandoo wa kit...
 

No comments:
Post a Comment