Grumman
Gulfstream IV. Ndege ya tume ya dunia ya kudhibiti madawa ya kulevya
ulimwenguni kote (WODEC) iliyotumiwa na Daktari wa Tume ya Dunia Dr
Aboubakar Dieudonné kutoka Kameruni: kwenda Sittard nchini Uholanzi,
kutafuta DNA ya John Murphy. Na iliyotumiwa na Vijana wa Tume kwenda
Guadalajara nchini Meksiko, kutetea afya na amani ya dunia.
Grumman
Gulfstream IV na Grumman Gulfstream III, za Tume ya Dunia na Kolonia
Santita kwa mpangilio huo, ni miongoni mwa ndege binafsi zilizotumika
katika kitabu cha KOLONIA SANTITA. G-III ilitumika kwenda kumchukua
Kachero wa Kolonia Santita Giovanna Garcia jijini Dar, baada ya
kushindwa kumnasa John Murphy kwa miwani; na ndiyo iliyotumika kumpeleka
Garcia na Kimbunga Mexico City nchini Meksiko, baada ya Operation
Kimbunga kukamilika. G-IV ilifanya kazi zote za tume katika kipindi
chote cha Operation Devil Cross: Sittard, Mexico City, New York,
Guadalajara, Vienna, mpaka Oslo nchini Norwe.
No comments:
Post a Comment