Sunday, 18 December 2016

Biashara Kuu ya Kolonia Santita Inayowaingizia Mamafia wa Amerika ya Kusini Dola Bilioni 40 kwa Mwaka

Kilo 625 za majani ya koka hutengeneza kilo 2.5 za mashudu ya kokeini (‘cocaine base’) ambayo baadaye hutengeneza kilo 1 ya kokeini isiyokuwa na doa (safi) katika hali ya kawaida ya unga mweupe! Leo asilimia 10 ya kokeini hutoka Bolivia, 29 hutoka Peru na 61 hutoka Kolombia. Mamafia wa Kolombia hupokea bidhaa katika hatua ya mashata – mashudu – na kumalizia uchakataji wa usafishaji katika vinu vya kusafishia madawa vya msituni, na kuuza takriban asilimia 100 ya ‘Cocaine hydrochloride’ au kokeini.

Zipo njia mbili kuu za kikemia zinazohitajika kubadili majani ya koka kuwa kokeini na njia hizo ni za bei nafuu kabisa. Majani mabichi hulowekwa ndani ya pipa kubwa la asidi (asidi ya betri inaweza kufaa pia) ambayo hufyonza kokeini kutoka katika majani hayo. Majani hayo kisha hukamuliwa na kutupwa na kuacha kitu kama uji au supu ya rangi ya kahawia hivi. Hii huchanganywa na pombe, au mafuta ya taa, ambapo baadaye hubadilika na kuwa kemikali za alkaloidi. Kisha kemikali hizi hukwanguliwa na kuchanganywa na alkali kali zaidi, kama vile madini ya magadi ya soda (‘sodium bicarbonate’ kwa utaalamu zaidi).

Mchanganyiko huu husababisha kutokea kwa mashudu meupe ya kokeini – mashata ya kawaida au ‘coca paste’ au ‘coca base’. Hiki ndicho kiwango cha kawaida cha biashara ya kokeini katika bara la Amerika ya Kusini. Hiki ndicho mamafia wa Kolonia Santita hununua kutoka kwa wakulima. Kilo 250 za majani ya koka zimegeuka kuwa kilo 1 ya mashudu ya kokeini, ambayo baadaye husafirishwa kutoka porini kwa njia za kimafia mpaka kiwandani kutengeneza kokeini.

1 comment:

  1. Kadiri unavyozidi kupanda juu ndivyo utakavyoanguka vibaya. Kadiri unavyozidi kutumia madawa ya kulevya ndivyo madhara yake yatakavyokuwa makubwa. Hivyo acha, wakati bado ni mapema.

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...