Tuesday, 29 November 2016

Wanaosema Hawajui Wanaojua Hawasemi

Panthera Tigrisi akimpiga mkwara John Murphy katika kasri la Benson Bennett la Salina Cruz, Oaxaca, nchini Meksiko. Badala ya kufumba macho kwa kuyakodoa, John Murphy alifumbua macho kwa kuyakodoa.

Fumba macho kwa kuyakodoa ni kutunza siri milele. Ulichokiona usikiseme daima maana ukikisema hakika utakufa. Las Vegas ni ofisi ya siri ya Panthera Tigrisi, kiongozi wa Kolonia Santita. Kilichofanyika pale kilibakia pale. 


Ukiona kitu ambacho hukupaswa kuona, au ukisikia kitu ambacho hukupaswa kusikia, fumba macho kwa kuyakodoa! Ulichokiona au kukisikia usikiseme leo na hata milele. Jifanye hukuona kitu, hukusikia kitu. Ukifumbua macho kwa kuyakodoa utapata matatizo, makubwa.

2 comments:

  1. Murphy aliambiwa na Panthera Tigrisi afumbe macho kwa kuyakodoa, yeye akafumbua macho kwa kuyakodoa. Fikiria nini kilitokea baada ya hapo.

    ReplyDelete
  2. Murphy alikuwa na hasira sana na Panthera Tigrisi (El Tigre) kwa sababu ya Radia. Badala ya Murphy kufumba macho kwa kuyakodoa, Panthera Tigrisi ndiye aliyefumba macho kwa kuyakodoa mwenyewe!

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...