Kitu cha kwanza kufanyika mwanadamu anapozaliwa ni kuvuta pumzi ya 
kwanza katika mapafu ya mwili wake. Cha mwisho kufanyika kabla ya kufa 
ni kutoa pumzi ya mwisho katika mapafu ya mwili wake. Pumzi iliyoingia 
kwanza baada ya kuzaliwa, itakuwa ya mwisho kutoka kabla ya kufa. Pumzi 
ni bora kuliko muda halafu pumzi ni uhai. Bila uhai watu hawataweza 
kusherehekea mwaka mpya au kufanya chochote. Likumbuke jina la Mwenyezi Mungu katika kila pumzi unayoingiza na kutoa. 
 
 Kwa nini watu wana kawaida ya kuona thamani ya mtu baada ya mtu 
kufariki? Kwa nini watu wana kawaida ya kuona thamani ya pumzi katika 
kipindi ambacho mtu hana uwezo tena wa kuvuta hewa? Nini thamani ya 
pumzi? Thamani ya pumzi ni kukufanya uwe wewe na si udongo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Roho Yako
289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...
- 
KITENDAWILI CHA KOLONIA SANTITA Shilingi milioni moja za Kitanzania kushindaniwa ndani ya miezi sita kuanzia leo Swali: Kila namba ...
 - 
Mpelelezi wa Tume ya Dunia kutoka Jerusalem, Israeli, Kanali Daniel ‘Yehuda Ben-Asher’ Ebenezer, Daniel Yehuda, alikuwa komandoo wa kit...
 

Biblia inatuambia kuwa tuombe bila kukoma (1 Wathesalonike 5:17). Lakini tutaombaje bila kukoma? Njia mojawapo ya kufanya hivyo ni kutumia ‘maombi ya pumzi’ kila siku kama ambavyo Wakristo wengi wamekuwa wakifanya kwa karne nyingi. Unachagua sentensi fupi au maneno rahisi kuhusu Yesu unayoweza kuyasema na kuyarudia kimoyomoyo kila siku katika kila pumzi inayoingia na kutoka ndani ya mapafu yako. Kwa mfano: “Asante Yesu.” “U pamoja nami.” “Nataka kukujua.” “Napokea neema yako.” “Nakutegemea wewe.” “Mimi ni wako.” “Nisaidie nikuamini.” “U Mungu wangu.” “Naishi kwa ajili yako.” “Nisamehe dhambi zangu zote.” Fundisha akili yako kumkumbuka Mungu kila wakati.
ReplyDelete‘Kusherehekea’ maana yake ni kumsifu na kumshukuru Mungu kila wakati, pumzi inapoingia na kutoka ndani ya mapafu yako.
ReplyDelete