Monday, 7 November 2016

Jitetee!

198. Huna mama huna mtetezi. Jitetee!

Mama anaweza kufa ili mwanawe aishi, anaweza kufunga na kuomba ili mwanawe Mungu amsaidie ashinde mtihani wake, anaweza kulala njaa ili mwanawe ale, anaweza kujitolea vitu vingi au mambo mengi katika maisha yake ili mwanawe aishi vizuri, anaweza kuingia dhambini ili mwanawe asamehewe.

Kama huna mama, kama mama yako alishafariki, au kama yupo lakini hakujali, hata kama baba yako yupo au hayupo, mafanikio yako yatatokana na juhudi zako mwenyewe.

Isipite siku hata moja katika maisha yako bila kusema hata kimoyomoyo kwa wazazi wako na kwa watu wote wanaokupenda kwamba unawapenda, kwani siku moja hawatakuwepo tena.

http://www.facebook.com/koloniasantita

2 comments:

  1. Hata wahenga walisema, “Mtegemea cha nduguye hufa maskini.”

    ReplyDelete
  2. Mama anaweza kuingia dhambini ili mwanawe asamehewe (kwa mfano anaweza kwenda kwa mganga wa kienyeji kwa ajili ya mafanikio ya mwanawe, na kadhalika).

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...