Monday, 14 November 2016

Jikusuru Kuujua Ukweli

199. Utajiri una changamoto nyingi. Yesu alisema ni rahisi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu. Hakusema msomi. Usiwe mwendanguu. Jikusuru kuujua ukweli.

Usiwe mwendanguu (usiwe mtu aliyekata tamaa kabisa). Jikusuru (jitahidi kwa kadiri ya uwezo wako wote) kuujua ukweli.

Lakini ukweli ni upi? Ukweli ni kwamba utajiri una changamoto nyingi kuupata na kuudumisha pia kuliko usomi na kwamba ukweli ni amani ya Mungu katika moyo wa mwanadamu. Heri msomi kuliko tajiri – Heri yule aliyesoma kuliko tajiri asiyesoma au yule aliyesoma kuliko vile alivyosoma tajiri au tajiri asiyesoma au aliyesoma lakini asiyekuwa na tamaa kabisa na dunia hii ambaye kukosa kwake tamaa na dunia hii kunamfanya msomi. Ndivyo Kristo anavyomaanisha. Si kwamba tajiri hawezi kuuona ufalme wa mbinguni. Ibrahimu, Isaka, Yakobo, Yusufu, Daudi, Sulemani, Yehoshafati, Hezekia, Zakayo, Yoana, Susana, na Lidia watauona ufalme wa mbinguni na walikuwa matajiri. Mali zao zilivyozidi hawakuangalia moyoni, hawakuwa na tamaa kabisa na dunia hii, bali walimtumaini Mungu kwa kila kitu walichokuwa nacho. Anaweza. Lakini asiipende dunia bali ayapende mambo ya ufalme wa Mungu kwa moyo wake wote.

http://www.facebook.com/koloniasantita

4 comments:

  1. Yoana mkewe Kuza (wakili wake Herode) pamoja na Susana walihubiri injili na walitoa mchango mkubwa katika mazishi ya Yesu Kristo pamoja na Mariamu Magdalene; Yusufu ‘Mwana wa Faraja’ aliuza shamba lake na kupeleka fedha miguuni pa mitume kwa ajili ya injili; na Lidia alianzisha kanisa la kwanza katika bara la Ulaya nyumbani kwake.

    ReplyDelete
  2. Hata kama umetajirika kiasi gani mpe Mungu kipaumbele cha kwanza katika kila jambo unalofanya. Toa zaka na sadaka na jitolee katika mambo yote yanayompendeza Mungu.

    ReplyDelete
  3. Mungu anataka tuwe na mtazamo wa ‘kila kitu kinawezekana juu ya jua’ na si ‘kila kitu kinawezekana chini ya jua’.

    ReplyDelete
  4. Tajiri asiyesoma lakini anayejali mambo ya ufalme wa Mungu kuliko anavyoijali dunia au yule aliyesoma lakini anayejali mambo ya ufalme wa Mungu kuliko anavyoijali dunia ni msomi. Anaweza kuuona ufalme wa Mungu.

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...