Monday, 14 November 2016

Chumba cha John Murphy

Chumba cha John Murphy katika Hoteli ya Sophie Amalie jijini Copenhagen, iliyoko katika mtaa uitwao Sankt Annæ Plads, John Murphy alipofikia badala ya Hoteli ya Astoria ambapo magaidi wa Kolonia Santita wangemmaliza.

Sophie Amalie Hotel ni hoteli ya kisasa ya kimataifa yenye hadhi ya nyota nne daraja la kwanza iliyoko jirani na Kasri la Kifalme la Amalienborg, kumbukumbu ya malkia wa karne ya kumi na saba wa Denmaki Malkia Sophie Amalie. Murphy alikaa Sophie Amalie Hotel chumba namba 117 kwa dakika 45 – kabla ya kutuma watu baadaye kwenda kuchukua mizigo yake na kuipeleka Makao Makuu ya Tume ya Dunia Vesterbrogade – kabla ya kuhamia Hellerup (kaskazini ya Copenhagen Mjini, au ‘Indre By’) katika nyumba ya siri ya mpelelezi wa Tume ya Dunia Frederik Mogens kutoka Denmaki.

No comments:

Post a Comment

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...