Tuesday, 11 October 2016
Kisiwa cha Saltholm
Saltholm ni kisiwa cha 21 kwa ukubwa kuliko vyote 406 vya Denmaki. Kipo katika Ukanda wa Bahari wa Øresund, unaoiunganisha Bahari ya Baltiki katika Bahari ya Atlantiki kupitia Kattegat, Skagerrak na Bahari ya Kaskazini; Daniel Yehuda, mpelelezi wa Tume ya Dunia kutoka Israeli, alipopelekwa na magaidi wa Kolonia Santita baada ya kutekwa katika Uwanja wa Ndege wa Copenhagen.
Daniel Yehuda, mpelelezi mashuhuri wa Tume ya Dunia kutoka Kidon (kitengo cha mauti na utekaji nyara cha shirika la kijasusi la Mossad la Israeli) alipotekwa na magaidi wa Kolonia Santita alipelekwa Saltholm kupitia Ghuba ya Køge na Dragør katika Manispaa ya Tårnby. Pembeni mwa kisiwa, kiasi cha meta kama mia nne hivi kutoka ufukoni – maadui walipoegesha boti yao – kulikuwa na nyumba ya kawaida ya vyumba viwili vikubwa vya kulala, choo, bafu, sebule na sehemu kubwa ya kuhifadhia vitu; iliyokuwa na ukuta wa rangi ya njano, kama nyumba nyingi za Dragør. Ilikuwa na vigae vikuukuu vya kijani. Haikuwa na ukuta wa ua. Ilikuwa na seng’enge na miti mingi (nje na ndani ya seng’enge hiyo) na geti kubwa la chuma kwa upande wa kusini, ambako ndiko maadui walikuwa wakitokea na Yehuda. Nje kulikuwa na zizi kubwa la ng’ombe, na hifadhi ya ndege (kama kinega, kubo, mpasuasanda na kinegwa – jamii ya mbayuwayu), na nyumba nyingine kwa mbali (kama kilometa moja au zaidi kidogo) ya mwangalizi wa kisiwa, na miamba michache (hasa karibu na ufuko) na miti mirefu ya njano (inayoteleza) ya hapa na pale ya miparamuzi. Matatizo aliyoyapata Yehuda yalikuwa makubwa. Lakini bila matatizo hayo Radia Hosni angeuwawa usiku wa siku hiyo bila kukosa, na John Murphy angeuwawa na magaidi wasiojulikana. Vijana wa Tume wasingejua kama Kolonia Santita ndiyo waliyohusika na ulipuaji wa ndege ya shirika la ndege la Ufaransa, kama Daniel Yehuda asingetekwa na magaidi wa Kolonia Santita. Kutekwa kwa Yehuda kulikuwa na faida.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Roho Yako
289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...
- 
KITENDAWILI CHA KOLONIA SANTITA Shilingi milioni moja za Kitanzania kushindaniwa ndani ya miezi sita kuanzia leo Swali: Kila namba ...
 - 
Mpelelezi wa Tume ya Dunia kutoka Jerusalem, Israeli, Kanali Daniel ‘Yehuda Ben-Asher’ Ebenezer, Daniel Yehuda, alikuwa komandoo wa kit...
 

Saltholm is a Danish island in the Øresund, the strait that separates Denmark and Sweden. It is located to the east of the Danish island of Amager in Tårnby municipality and lies just to the west of the sea border between Denmark and Sweden. – Wikipedia
ReplyDelete