Macho ya tai yana nguvu mara nne zaidi ya macho ya mwanadamu. Tai ana
 uwezo wa kuona hadi umbali wa kilometa themanini bila matatizo yoyote. 
Ana uwezo wa kuruka hadi futi elfu kumi, na ana uwezo wa kukimbia hadi 
mwendokasi wa kilometa mia moja na ishirini kwa saa. Kihekima, wale tu 
wanaoweza kuona mbali kama tai ndiyo watakaouweza msamaha.
 Lakini wale wenye mabawa ya kuku, wale ambao hawawezi kuruka wala kuona
 mbali, watapata taabu sana kuijua radhi. Kwa hiyo, wanapaswa kukua. 
Ukiwa mnyenyekevu wa moyo hutamchukia adui yako.
Msamaha si jambo 
dogo. Watu wadogo, watu wenye uwezo mdogo wa kufikiri, hawawezi 
kupambana na changamoto za msamaha. Msamaha ni kwa ajili ya watu wenye 
macho kama ya tai wanaoweza kuona mbali ambao wako tayari kushindwa vita
 ili washinde vita. Hewa inaingia ndani ya mapafu na kutoka; chakula 
kinaingia ndani ya mwili na kutoka; mwanamasumbwi anapigana bila 
kugombana; injini ya gari haiwezi kusukuma gari mbele au nyuma bila 
kutoa hewa katika paipu ya ekzosi. Lakini kile kinachoingia moyoni mwako
 hakitoki! Maumivu yanapoingia ndani ya moyo yanapaswa kutoka nje kama 
yalivyoingia kwa sababu, yasipotoka yatatengeneza sumu ndani ya moyo 
wako na yatatengeneza sumu ndani ya roho yako pia. Sumu hiyo 
itahatarisha safari yako ya mbinguni na Mungu hatakusamehe tena. Badala 
ya yule aliyekukosea kuumia, utaumia wewe uliyekosewa. Yesu anaposema 
samehe saba mara sabini hatanii. Usiposamehe, hutasamehewa. 

Mungu hapendi hasira kwa sababu ni vigumu kutokutenda dhambi ukiwa na hasira.
ReplyDelete