Friday, 6 February 2015

Pasifiki

Bahari kubwa kuliko zote ulimwenguni inayotumiwa na majambazi wa Amerika ya Kusini na Kaskazini kusafirisha madawa ya kulevya duniani kote – Pasifiki – meli saba za Kolonia Santita zilipokamatwa zikiwa njiani kuelekea India, Marekani, Afrika Kusini na Ginebisau, Kiongozi wa Kolonia Santita Panthera Tigrisi alipokamatwa akiwa njiani kuelekea Kolombia na Guatemala.

http://www.enockmaregesi.wordpress.com

1 comment:

  1. Meli ya kwanza kuondoka katika Bandari ya Salina Cruz kusini mwa Meksiko katika Bahari ya Pasifiki ni 'La Diosa de los Mares', 'Mungu wa Bahari', au 'Goddess of the Seas', Tani 6000, iliyoondoka saa tisa kamili usiku kuelekea Miami nchini Marekani; wakati ya mwisho kuondoka ilikuwa CSS ('Colonia Santita of the Seas', Tani 10000), na SPD ('El Silencio Depredador del Profundo', 'Mnyama Mtulivu wa Kina Kirefu', 'The Silent Predator of the Deep' – nyambizi ya Panthera Tigrisi), zilizoondoka saa kumi na moja alfajiri kuelekea Guatemala na Kolombia. Salina Cruz ni sehemu iliyopo kandokando mwa Bahari ya Pasifiki kusini kabisa mwa Meksiko na kaskazini-mashariki kwa Reparo Jicara katika jimbo la Oaxaca. Kambi ya Panthera Tigrisi ilijengwa ndani ya Msitu wa Benson Bennett – katika ufuko wa bahari kubwa kuliko zote ulimwenguni, iliyopuliza hewa na kuyumbisha miti anuai juu ya maabara kubwa kuliko zote katika Hemisifia ya Magharibi; ya kokeini, heroini, bangi, eksitasi na hielo ya China na Kolombia. Panthera Tigrisi alikamatwa katika Bahari ya Pasifiki. Kahima Kankiriho alikamatwa katika Msitu wa Bennett.

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...