CERN, makao makuu ya shirika la utafiti wa nyuklia la bara la Ulaya karibu na Geneva nchini Uswisi, Kiongozi wa Kanda ya Afrika ya Kusini ya Tume ya Dunia Kamishna Profesa Justin Mafuru wa Tanzania alipokuwa akifanya kazi, katika jitihada za kujibu maswali mazito ya mwanzo wa ulimwengu wetu kwa kutengeneza mazingira ya mwanzo kabisa ya mlipuko wa 'Big Bang'.
http://www.enockmaregesi.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Roho Yako
289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...
- 
KITENDAWILI CHA KOLONIA SANTITA Shilingi milioni moja za Kitanzania kushindaniwa ndani ya miezi sita kuanzia leo Swali: Kila namba ...
 - 
Mpelelezi wa Tume ya Dunia kutoka Jerusalem, Israeli, Kanali Daniel ‘Yehuda Ben-Asher’ Ebenezer, Daniel Yehuda, alikuwa komandoo wa kit...
 

Kiongozi wa kanda ya Afrika ya Kusini ya Tume ya Dunia Kamishna Profesa Justin Mafuru, alijitolea maisha yake kufanya vitu viwili vya msingi kwa ajili ya dunia: Kukomesha madawa haramu ya kulevya nchini Tanzania na duniani kwa jumla, kupitia Tume ya Dunia, na kutafuta kupitia maabara za CERN ('Conseil Européen pour la Recherche Nucléaire') chembe ndogo ya 'higgs' ('Higgs Boson') inayosemekana kuhusika na uzito ('mass') wa chembe ndogo kumi na sita za atomu kasoro chembe ya mwanga; iliyopotea mara tu baada ya mlipuko wa ulimwengu wa 'Big Bang', miaka bilioni kumi na tatu nukta saba iliyopita kwa faida ya uanadamu.
ReplyDeleteMimi na wewe na vitu vyote ulimwenguni ni wazito kwa sababu ya 'Higgs Boson', inayojulikana pia kama 'The God’s Particle'. Wanasayansi wa CERN wamekuwa wakiitafuta 'higgs' (iliyojificha ndani ya 'higgs field') kwa zaidi ya miaka hamsini sasa, kwa bajeti ya pauni za Uingereza bilioni sita. Chembe ya 'higgs' ikipatikana itawajulisha wanasayansi jinsi ulimwengu unavyofanya kazi na jinsi ulivyoumbwa, na jibu la kitendawili cha 'Standard Model' litapatikana.
ReplyDeleteNdani ya sekunde moja baada ya ulimwengu wetu kuumbwa, miaka bilioni kumi na tatu nukta saba tano iliyopita, chembe zote ndogo zinazopatikana ndani ya atomu zilitengenezwa. Zote hizo zimeshapatikana isipokuwa 'Higgs Boson', na 'Higgs Boson' ndiyo ya muhimu kuliko zote.
ReplyDeleteKuna makusudi maalum mungu kuisicha higgs!
ReplyDelete