Monday, 20 October 2014

Roho Mtakatifu

107. Mwili wako una uwezo wa kujua kabla yako kitakachotokea baadaye. Kama una njaa kwa mfano, mwili wako utakwambia. Kama una kiu, mwili wako utakwambia. Kama unaumwa, mwili wako utakwambia. Kama kuna kitu kibaya kinatarajia kutokea katika maisha yako au katika maisha ya mtu mwingine, mwili wako utakwambia. Kuwa makini na alamu zinazotoka ndani ya mwili wako, kwani hizo ni ishara za Roho Mtakatifu kukuepusha na matatizo ya dunia hii.

http://www.facebook.com/koloniasantita

6 comments:

  1. Siku moja huko nchini Marekani mama mmoja aliamshwa usiku wa manane na jinamizi au ndoto ya kutisha. Shandalia iliyoning’inia chumbani kwa mtoto wake mchanga karibu na mlango ilianguka juu ya susu, kitanda cha mtoto, na kumuua! Saa ya redio pembeni mwa kitanda, akiwa bado yuko ndotoni, ilionyesha saa 10:35 za alfajiri. Kwa woga usio na kifani, yule mama, alipoamka, alimwamsha mumewe na kumwambia alichoota. Mumewe kwa bahati mbaya hakuwa muumini wa ndoto za kutisha, lakini alitaka kumwondolea shaka mkewe. Kwa hiyo alimwomba asiwe na hofu na alale, kwa sababu mtoto wao alikuwa salama.

    Lakini yule mama hakupata tena usingizi. Hivyo alisimama kisha akaenda chumbani kwa mtoto wao na kumchukua mtoto, kisha akarudi naye mkapa kitandani kwao na kumlaza pembeni yake, halafu ndipo akalala tena.

    Baadaye usiku, wazazi wote wawili waliamshwa tena. Lakini safari hii wakaamshwa na sauti kali ya dhoruba. Walisikia sauti kali ikitokea katika chumba cha jirani, hivyo wote wakakurupuka na kukimbia mpaka chumbani kwa mtoto wao. Shandalia iliyokuwa ikining’inia juu ya kitanda cha mtoto kumbe ilikatika na kuanguka juu ya susu, ambapo kwa bahati nzuri mtoto hakuwepo. Yule mama alivyoangalia saa, ilionyesha saa 10:35 za alfajiri.

    Mfano huu wa jinsi Roho Mtakatifu anavyoweza kumsaidia mtu na kumwepusha na ajali au matatizo yoyote ni mzuri sana, asante kwa maisha yaliyookolewa. Kama angeidharau hii ndoto, yule mama angejuta maisha yake yote.

    ReplyDelete
  2. Kujua nini kitatokea kesho, au kesho kutwa, au kujua jinsi usaili wako wa kazi utakavyokuwa, au ni maswali gani utakayoulizwa kwenye mtihani kwa mfano, kutarahisisha sana maisha yetu. 'Madirisha' madogo katika kipindi cha saa za usoni hufunguka mara kwa mara katika maisha yetu, kimiujiza na bila kutegemea. Hudokeza kidogo jinsi tukio fulani, au hali fulani, au kitu fulani kitakavyotokea katika kipindi cha wakati ujao bila sisi wenyewe kujua. Hali hii hujulikana kama jakamoyo. Jakamoyo ni sanaa ya kubashiri vitu visivyojulikana. Kazi yake ni kutuhadharisha na kutusaidia! Kujua mapema hatari iliyoko mbele yako inamaanisha kuwa na uwezo wa kujilinda kutokana na hatari hiyo, na kuwa na uwezo wa kuepuka mitego. Jakamoyo huweza kumtokea mtu katika hali ya 'maono', au 'mwako wa mwanga' (yaani kufumba na kufumbua). Mara nyingi huonekana kama ndoto. Hutokea wakati mtu amelala usingizi. Ikitokea wakati mtu yuko macho, wakati mwingine huendana na misisimko ya mwili kabla ya mwako, ikiwa na maana ya kumfanya mtu awe makini na kitu chochote kinachotarajia kutokea. Ndiyo maana baadhi ya watu utakuta wakisema wanaumwa tumbo, kifua au kichwa cha ghafla katika kipindi ambacho taswira ya tukio fulani inakuwa ikitokea akilini mwao, ikiwaambia waende mahali fulani bila kukosa kwa mfano, na kadhalika. Hakuna mtu anaweza kufanya jakamoyo imtokee. Hutokea yenyewe muda wowote kuleta ujumbe, kuhusiana na matukio ya wakati ujao. Kamwe usipuuze wito wa moyo wako.

    ReplyDelete
  3. Roho mtakatifu ndie kiongozi wa kila mtu ijapokua hata shetani anatuongoza pia,lakin watu wanapaswa kuwa na utashi wa kujua nani ni roho mzuri na nani ni roho mbaya kwa mawazo yangu mm watu wanapaswa kumfuata roho mtakatifu

    ReplyDelete
  4. Msemo wa ‘Majuto ni mjukuu’ hauna maana yoyote kama utamsikiliza na kumfuata Roho Mtakatifu. Ukiwa na Roho Mtakatifu hakuna kujuta.

    ReplyDelete
  5. Do not ignore the calling of your heart.

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...