BFR – kiatu cha kijeshi kutoka Singapori chenye uwezo wa kuzuia risasi na mabomu ya ardhini – kilichookoa maisha ya mpelelezi wa Tume ya Dunia kutoka Tunisia Sajini Radia Hosni, Vijana wa Tume walipokuwa wakipambana na Kolonia Santita huko Frederiksberg (manispaa ndani ya manispaa ya Copenhagen), nchini Denmaki.
http://www.enockmaregesi.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Roho Yako
289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...
- 
KITENDAWILI CHA KOLONIA SANTITA Shilingi milioni moja za Kitanzania kushindaniwa ndani ya miezi sita kuanzia leo Swali: Kila namba ...
 - 
Mpelelezi wa Tume ya Dunia kutoka Jerusalem, Israeli, Kanali Daniel ‘Yehuda Ben-Asher’ Ebenezer, Daniel Yehuda, alikuwa komandoo wa kit...
 

“Maadui, wale wa kaskazini, walijua Radia hakuuwawa. Walijua alipigwa miguuni. Miguu ndiyo iliyobaki nyuma wakati risasi zikimpiga na kumsindikiza nje. Hivyo (walijua) Radia hangeweza kukimbia, hata kutembea, alipodondoka. Wawili, kwa pupa, walikimbia (kipindi hicho Murphy ndipo akimiminiwa risasi katika ghorofa ya tatu na yule adui mfupi) na kupanda ukuta aliporukia Radia kusudi wammalize kabisa kijana wa tume kwa bunduki zao. Walipotokeza juu, wale walinzi wawili, hawakuwaona kabisa Vijana wa Tume. Radia, Yehuda na Mogens walikuwa bado wamebana wakiwasubiri tu watokeze. Walipotokeza, Radia, Yehuda na Mogens – kwa pamoja – walifyatua bunduki. Maadui wakafa, palepale, wote; halafu Radia, Mogens na Yehuda wakakimbia mpaka upande wa kusini na kujaribu kutumbukia uani kupitia huko au upande wa mashariki. Radia hakuwa na maumivu yoyote. Kipindi anapigwa, risasi hazikumuumiza. Alikuwa na fulana nzito ya kuzuia risasi; na viatu, BFR, maalumu kutoka Singapori, vyenye uwezo wa kuzuia risasi na mabomu.” –Kolonia Santita 160-161
ReplyDeleteViatu vya kijeshi vya BFR (‘Blast and Fragment Resistant’) kutoka Singapori, vilichangia kwa kiasi kikubwa kukamilika kwa operesheni ndogo ya Tume ya Dunia Operesheni Kimbunga; bila maafa kwa Vijana wa Tume au kwa Tume ya Dunia.
ReplyDelete