Bustani za Tivoli, katikati ya kituo kikubwa cha treni cha Hovedbanegård
 na kituo kikubwa cha mabasi cha Rådhuspladsen, ni bustani kubwa za 
michezo na mapumziko za Copenhagen. Bustani hizi ndizo zilizotumika 
kuwapoteza majambazi wa Kolonia Santita katika harakati za kumwokoa 
Daniel Yehuda wa bandia, katika Machafuko ya Sheraton jijini Copenhagen.
http://www.enockmaregesi.com  
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Roho Yako
289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...
- 
KITENDAWILI CHA KOLONIA SANTITA Shilingi milioni moja za Kitanzania kushindaniwa ndani ya miezi sita kuanzia leo Swali: Kila namba ...
 - 
Mpelelezi wa Tume ya Dunia kutoka Jerusalem, Israeli, Kanali Daniel ‘Yehuda Ben-Asher’ Ebenezer, Daniel Yehuda, alikuwa komandoo wa kit...
 

Majambazi wa Kolonia Santita Regner Steiner ('Kimbunga') na Ulla Wagner ('Death Queen'); walivyokimbia wakiwa ndani ya magari mawili ya kihuni, Polisi wa Tume na wa Copenhagen waliwaona vizuri. Polisi waliingia katika magari yao kwa pupa na kuwafukuza maadui kwa nguvu zao zote, lakini maadui wakawashinda nguvu. Maadui walionekana kuwa mafundi stadi wa kuendesha magari, bila hata kujali watu na magari mengine mabarabarani. Kimbunga alijizungusha nje ya Bustani za Tivoli kwa muda mrefu na hatimaye kujikuta akiwauza kabisa polisi wa tume na polisi wa Copenhagen; lakini Ulla, aliyekimbilia upande mwingine wa Barabara ya Søgade, hakufika mbali hata hivyo. Alizingirwa, ghafla, na magari mengine ya polisi ambayo kwa kipindi kile yalikuwa yakitokea katika kituo kikuu cha polisi cha Tume ya Dunia kilichopo Århusgade.
ReplyDelete