Maabara ya Taifa ya Nguvu za Kinyukilia,
Los Alamos, New Mexico, Marekani.
Mabomu ya atomiki ya 'Fat Man' na 'Little Boy' ya Marekani, yaliyoanguka Nagasaki na Hiroshima (kutokea Tinian, Marianas, Bahari ya Pasifiki) nchini Japani Agosti 1945, yalipoundwa. Na ndipo malighafi ya nyukilia ya 'Plutonium-239' ya Kolonia Santita, ilipoibwa na Kiongozi wa Kateli ya Madawa ya Kulevya ya Guanajuato Roberto Mosquera Portocarrero ('El Padrino', 'The Godfather'), adui mkubwa wa Panthera Tigrisi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Roho Yako
289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...

-
Mpelelezi wa Tume ya Dunia kutoka Jerusalem, Israeli, Kanali Daniel ‘Yehuda Ben-Asher’ Ebenezer, Daniel Yehuda, alikuwa komandoo wa kit...
-
Uwanja wa Ndege wa Copenhagen-Roskilde: uliotumiwa na Tume ya Dunia na Kolonia Santita kwa pamoja – kilometa tisa kutoka katika Kanisa ...
Martin Turner Smith – mwanafizikia wa Kolonia Santita wa New Mexico nchini Marekani – ndiye aliyeiba 'Plutonium-239' kutoka kwa El Padrino, na hivyo kuchochea ugomvi kati ya Kateli ya Kolonia Santita na Kateli ya Guanajuato (genge la madawa ya kulevya la Tijuana na Guanajuato) wa nani atawale ukiritimba wa kokeini wa Kolombia; dhidi ya vyama haramu vya msituni vya Amerika ya Kusini. Kilo kumi za 'plutonium' (Kolonia Santita walikuwa na kilo moja) huweza kutengeneza bomu moja la nyukilia kama la Nagasaki, na huweza kutengeneza mafuta ya kuendesha nyambizi ya kijeshi kwa umbali wa kilometa 250000. Watu wanasema sekunde chache kabla ya kufa utayaona maisha yako mbele ya macho yako. Bomu la nyukilia likianguka (na kulipuka) mahali ulipo, hutajua uliwahi kuishi.
ReplyDeleteBonge la picha, hongera sana Enock.
ReplyDeleteAsante, David.
DeletePicha iko relevant na story ya kitabu. Like it.
ReplyDeletei luv the pic
ReplyDeleteViwanda vya kikemia ni hatari kwa afya za binadamu.
ReplyDelete