WODEC Mexico City
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Roho Yako
289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...

-
Mpelelezi wa Tume ya Dunia kutoka Jerusalem, Israeli, Kanali Daniel ‘Yehuda Ben-Asher’ Ebenezer, Daniel Yehuda, alikuwa komandoo wa kit...
-
Uwanja wa Ndege wa Copenhagen-Roskilde: uliotumiwa na Tume ya Dunia na Kolonia Santita kwa pamoja – kilometa tisa kutoka katika Kanisa ...
Makao Makuu ya Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya nchini Meksiko na katika nchi za Latino. Zona Rosa (Kanda ya Pinki) ndipo shughuli zote za Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya mjini Mexico City zinapofanyika; na ndipo ofisi ya Kamishna wa Kanda ya Amerika ya Kaskazini ya Tume ya Dunia Profesa Randall Buchanan Ortega ilipo. Ni kitongoji cha matajiri na ofisi (zikiwemo ofisi za kimataifa) magharibi mwa kitovu cha kihistoria cha Mexico City cha Centro Histórico. Hujulikana kwa kuwa na watu wengi wa Korea, kwa maduka, kwa starehe na kwa mashoga, mitaa yake mingi ikiwa na majina ya heshima ya miji ya bara la Ulaya. WODEC Mexico City (Ofisi ya Tume ya Dunia) iko katika kona ya kusini ya Zona Rosa, karibu na Kituo cha Metro cha Insurgentes, na Barabara Kuu ya Chapultepec. Zona Rosa ni sawa na Posta Mpya kwa Dar es Salaam hapa kwetu Tanzania.
ReplyDelete