Mexico City ikiwa chini ya ulinzi mkali wa majeshi binafsi yasiyo rasmi ya Kolonia Santita, Jumatano asubuhi; Vijana wa Tume wanakutana na Debbie Patrocinio Abrego, mtoto wa Rais wa Meksiko; na Lisa Madrazo Graciano, mtoto wa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Meksiko; San Ángel, Álvaro Obregón, Mexico City.
Vijana wa Tume wamefurahi kumwona Debbie. Wanahisi anahusika na Kolonia Santita. Kupata kitu ambacho hujawahi kupata lazima ufanye kitu ambacho hujawahi kufanya. Debbie ana siri itakayobadilisha historia ya Kolonia Santita. Lisa ana gari (Ferrari Testarossa juu) itakayobadilisha historia ya Tume ya Dunia. Kigumu kuliko vyote ni kizuri kuliko vyote. Vijana wa Tume hawatarudi salama. Mmoja wao atapata matatizo.
Vijana wa Tume wanaingia Meksiko kupambana na shirika katili la madawa ya kulevya la Kolonia Santita, CS-14, kubwa kuliko yote katika Hemisifia ya Magharibi, Jumatatu usiku wa manane katika mazingira ya kutatanisha.
ReplyDeleteMatairi ya gari ya Lisa ni makubwa kidogo kulinganisha na Ferrari Testarossa za kawaida. Ferrari Testarossa za mwanzo zilikuwa na matairi ya Michellin TRX, katika saizi ya 240/45x415 kwa matairi ya mbele na 280/45x415 kwa matairi ya nyuma. Ferrari Testarossa ya Lisa ilikuwa na matairi ya Michellin Pilot Sport, katika saizi ya 285/40x19 kwa matairi ya mbele na 285/40ZR19 kwa matairi ya nyuma; yaliyotengenezwa Ufaransa barani Ulaya.
ReplyDelete285 – Upana wa tairi zima kwa nje na ndani kwa kipimo cha milimeta.
40 – Urefu wa ukuta wa tairi ('profile' au 'aspect ratio'), yaani 40% ya 285mm.
Z – Kiwango cha mwendo mkali na uwezo wa kudumu kwa muda mrefu.
R – Muundo wa ndani ya tairi wa 'Radial construction', au 'Radial-ply'.
19 – Kipenyo cha tairi na gurudumu ('rim') kwa inchi (au 'inches').
415 – Kipenyo cha tairi na gurudumu kwa milimeta (au 'millimeters').
Matairi yenye teknolojia ya Radial-ply (nyuzi za tairi zilizosukwa kwa mtiririko wa kutokea katikati ya kufikirika ya tairi na kusambaa tairi zima) husaidiana na breki ya upepo kwa nyuma ('rear wing spoiler') kukandamiza gari wakati wa mwendo mkali ili isiyumbe sana barabarani. Matairi ya Radial-ply ni imara (na hununulika sana) kwa zaidi ya asilimia 98 ya matairi yote. Gari ya Lisa hapo juu ni mfano tu wa gari ya Lisa.
Gari ya Lisa ilikuwa na uwezo wa kukimbia umbali kadhaa bila upepo licha ya matairi yake kuwa na kinga ya risasi ya inchi nne. Ilikuwa na kitu kinaitwa 'Self-supporting run-flat tyre' (au tekinolojia ya 'flat tyre') kilichokuwa na uwezo wa kufanya matairi ya Ferrari yakimbie (bila upepo kabisa) mpaka umbali wa kilometa themanini, kwa mwendo wa kilometa themanini kwa saa.
ReplyDelete