Monday, 31 December 2012

Dar

13. Katika jiji la Dar watu hawaendi kazini. Wanakwenda vitani. Wania kilicho chako ukidhulumiwa. Utajiri humpendelea anayejaribu.

http://www.facebook.com/koloniasantita

3 comments:

  1. Kiongozi wa ‘Wakombozi’ akitoa wosia kwa genge lake la madawa ya kulevya. Wania maana yake ni shindana. Shindana na kitu au mtu aliyekudhulumu kupata haki yako kwa njia za kidiplomasia.

    ReplyDelete
  2. Nakubaliana na hilo....! Utajiri haupendelei watu wanaochukulia vitu for granted!

    ReplyDelete
  3. Nchi zilizoendelea kwa mfano, haki ya mtu haiwezi kudhulumiwa halafu watu wakakaa kimya ... Wataitafuta hata kwa sheria. Ukifuja pesa ya serikali halafu ukashindwa kutoa maelezo mwafaka ya matumizi ya pesa hiyo, wananchi watatumia nguvu zao zote kuhakikisha unarudisha pesa yao (waliyofanya kazi kwa bidii kubwa kuitafuta); na ukishindwa utawajibika na pesa hiyo katika vyombo vya sheria.

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...