Monday, 12 February 2018

Shida na Raha

264. Tunaumbwa kwa mfano wa Mungu kupitia shida na raha, kwa sababu ya ukaidi wa asili yetu kama binadamu. Bila shida na raha hatutakomaa wala hatutakamilika. Wakati mwingine Mungu anatufinya ili tusikie.

Ukaidi ni asili ya binadamu. Si rahisi kuibadili, hadi ujue wewe ni nani na kwa nini ulizaliwa. Ukijua wewe ni nani na kwa nini ulizaliwa utaishi sawasawa na mapenzi ya Mungu kwa binadamu.

Wenye shida katika Bwana wamebarikiwa. Wenye furaha ni wale wasiokuwa na furaha.

Kidunia wenye furaha ndiyo tunaosema wamebarikiwa. Lakini Kimungu wenye furaha ni wale wasiokuwa na furaha kwa sasa, lakini wenye hakika ya kuwa na furaha kwa baadaye. Yaani, kidunia wenye shida katika Bwana ndiyo tunaosema wamebarikiwa. Fungua moyo wako, ili uwe mkunjufu na mnyenyekevu.

Chochote kinachotokea katika maisha yako Mungu anakupa njia ya kufika pale anapotaka ufike. Jifunze lugha ya maisha ambayo Mungu anajaribu kuongea na wewe.

No comments:

Post a Comment

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...