Thursday, 11 January 2018

Mjinga au Mpumbavu

Mtu akikuita mjinga au mpumbavu juu ya maisha yako usikasirike kwa sababu wewe si mjinga wala mpumbavu. Sema hapana kwa ndiyo nyingi kwa sababu hawapaswi kuingilia mambo ya mtu mwingine bila idhini ya Mwenyezi Mungu. Kuingilia mambo ya mtu mwingine bila idhini ya Mwenyezi Mungu ni dhambi, tena dhambi kubwa, ni kuvunja amri kuu ya kwanza ya Mungu.

Mungu ana mpango na maisha ya kila mtu hapa duniani bila kujali dini, jinsia, kabila, rangi, taifa, au umri, na kila mtu ni wa kipekee.

Usiingilie mambo ya mtu mwingine bila kibali kutoka kwa Mungu. Kuingilia mambo ya mtu mwingine bila kibali kutoka kwa Mungu ni dhambi. Dhambi hiyo itakuathiri. Hivyo, jali mambo yako – ya mwingine Mungu anayafanyia kazi – hadi utakapoitwa na Mungu kuingilia kati. Kuingilia kati mambo ya mtu mwingine kunaweza kuathiri mpango wa Mungu katika maisha yake. Hivyo, acha.

Kama John Doe ana matatizo katika maisha yake acha ayatatue mwenyewe. Akishindwa atakuomba ushauri au ataomba ushauri kutoka kanisani kama ni Mkristo, au msikitini kama Mwislamu, au kutoka katika nyumba yoyote ya ibada kulingana na imani yake. Mtu akikuomba ushauri mshauri kwa moyo wako wote, wala usimshauri kwa unafiki au kinyongo cha aina yoyote ile.

Wewe kuingilia mambo ya John ni sawa na kusema, “Mungu umeshindwa hebu ngoja na mimi nijaribu; ngoja niingilie kati kukusaidia juu ya maisha ya John Doe.” Hiyo ni dhambi. Tena ni dhambi kubwa. Unajifananisha na Mungu; kwamba Mungu wa John Doe ameshindwa kwa hiyo mungu wewe ndiye utakayemtatulia matatizo yake.

Amri kuu ya kwanza ya Mungu inasema, “Usiwe na miungu mingine ila mimi.” Kuingilia mambo ya John tayari umevunja amri ya kwanza ya Mungu kwa kujifanya Mungu. Mungu ana mpango na maisha ya John, na anatumia matatizo yake kumfikisha kwenye takdiri aliyompangia. Hivyo, wewe si Mungu, acha Mungu afanye kazi yake. Mungu akikuruhusu kuingilia kati, yaani John akiamua kwa hiari yake mwenyewe kukuomba msaada wa mawazo au ushauri, maana yake ni kwamba Mungu amekuchagua wewe kuwa sehemu ya mafanikio ya John Doe.

“Historia ya maisha yangu ni yangu. Wewe ni nani kusema historia yangu si ya kweli?” –Enock Maregesi

Umesikia mtaani kwamba mke wa kaka yako anatembea na teja, na ukathibitisha, lakini bila kaka yako au shemeji yako kujua. Je, utamwambia kaka yako? Je, utamwambia shemeji yako? Je, utawambia watu wengine? Jibu unalo.

No comments:

Post a Comment

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...