255.
Ukiwa maasumu (ukiwa mwema) hutakuwa na maarifa ya ulimwengu huu na
unataka kufanikiwa. Wale waliofanikiwa kutokana na maarifa ya ulimwengu
huu hawatakupenda.
Matajiri wengi wamefanikiwa kutokana na nguvu za giza. Ukitaka kufanikiwa kama wao na wewe hupendi nguvu za giza watakuchukia; watakuona huna akili. Kuwasaidia lazima wawe kama wewe; na kukusaidia lazima uwe kama wao.
Wao wamefanikiwa kwa nguvu za giza lakini wewe unataka kufanikiwa kwa nguvu za nuru kupitia nguvu za giza. Unadhani watakusaidia?
Wasaidie, kwa hekima. Bila hivyo, wewe na wao, hamtauona ufalme wa Mungu.
Unaambiwa uende kwa mganga wa kienyeji ili upate hela hutaki. Lakini unaomba hela kwa mtu aliyekwenda kwa mganga wa kienyeji na akapata hela. Ukishirikiana na mwizi, wewe pia ni mwizi.

No comments:
Post a Comment