Monday, 20 November 2017

Duniani Wawili Wawili

252. Duniani wawili wawili. Umewahi kujiuliza kwa nini? Kwa nini mtu afanane sana na mtu mwingine ambaye hata si ndugu yake na labda mmoja anakaa Kagera na mwingine Tanga? Au mmoja anakaa Rwanda na mwingine Tanzania?

Nguvu za Shetani zimejificha katika sehemu za siri za mwanadamu. Kujamiiana (tendo batili la ndoa) kunautia najisi mwili wako na roho yako pia, hasa wakati wa kumwaga manii; kwa sababu dhambi zote anazofanya mwanadamu ziko nje ya mwili wake isipokuwa dhambi ya uzinzi, ambaye mungu wake anaitwa Asmodeus. Asmodeus maana yake ni Kiumbe cha Hukumu. Kutokana na dhambi ya uzinzi ndiyo maana Mungu akauhukumu kwa moto mji wa Sodoma, na miji mingine minne ya kipindi hicho.

Tunapokuwa tumelala mara nyingi tunaota ndoto tukifanya mapenzi, na watu tunaowajua au tusiowajua, hadi kileleni. Ndoto hizo ni za kishetani. Shetani hujigeuza na kuwa jini jike (Succubus) ambalo hufanya mapenzi na mwanamume kisha mwanamume kummwagia manii Succubus. Halafu Succubus huyohuyo hujigeuza na kuwa jini dume (Incubus) na kufanya mapenzi na mwanamke popote pale duniani, kwa lengo la kumwaga zile shahawa katika uchi wa mwanamke, hivyo kutia najisi mwili na roho ya mwanamke na mwanamume walioingiliwa na Incubus na Succubus kwa mpangilio huo.

Iwapo uliwahi kuota unafanya mapenzi na mwanamume, kuna uwezekano mkubwa ulifanya mapenzi na jini mahaba aitwaye Incubus; na iwapo uliwahi kuota unafanya mapenzi na mwanamke, kuna uwezekano mkubwa ulifanya mapenzi na jini mahaba aitwaye Succubus.

Succubus anapochukua shahawa za mwanamume na kujigeuza kuwa Incubus, huangalia ni mwanamke gani popote pale duniani yuko tayari kunasa mimba na bado hajafanya tendo la ndoa na mume au mpenzi wake. Kwa ruhusa ya Mwenyezi Mungu Incubus atasafiri kwa mwendo wa mwanga hadi kwa mwanamke huyo na kufanya naye mapenzi kwa njia ya ndoto, lakini lengo likiwa ni kummwagia zile shahawa alizozitoa kwa mwanamume, ili mwanamke anase mimba.

Miezi tisa baadaye, mtoto atakapozaliwa, baba halisi wa mtoto atakuwa si mume au mpenzi wa mama wa mtoto; na atafanana kivinasaba na watoto wa baba asiyejulikana, bila baba huyo au mtu mwingine yeyote yule kujua.

Lengo hasa la mpango huo ni Succubus na Incubus kunyonya nguvu za mwanamume na mwanamke (Succubus na Incubus hawanyonyi damu) hadi nguvu ziwaishe kabisa na wafariki dunia. Mtoto atakayezaliwa atakuwa na roho ya jini, atajulikana kama “cambion child”.

Kuna njia sita za kuondoa mapepo katika mwili wa mwanadamu: kwanza, kwa kukiri kwa Sakramenti; pili, kwa ishara takatifu ya msalaba au kwa kutamka Salamu ya Malaika kwa Mariamu mama yake Yesu na kwa Elizabeti mama yake Yohana Mbatizaji; tatu, kwa matumizi sahihi ya kupunga mapepo kama wafanyavyo wachungaji wengi; nne, kwa kuhamia mahali pengine tofauti kabisa na unapoishi; tano, kwa kutumia waganga wa kienyeji; na sita, kwa pepo kutengwa na mtu lakini kwa uangalifu wa watu watakatifu.

Kukiri kwa Sakramenti kunapatikana katika kitabu cha Yohana 20:21-23, katika Biblia, wakati Salamu ya Malaika Gabrieli kwa Mariamu mama yake Yesu na kwa Elizabeti mama yake Yohana Mbatizaji inapatikana katika kitabu cha Luka 1:28 na Luka 1:42 kwa mfuatano huo.

Katika njia ya nne ya kuondoa mapepo katika mwili wa mwanadamu, yaani kuhama kutoka sehemu moja kwenda nyingine kumkimbia Succubus au Incubus, kuna tatizo. Ukihamia mahali pengine tofauti na ulipokuwa ukiishi jini litabaki mahali ulipokuwa ukiishi mwanzo, lakini litawasumbua sana wale watakaokuwa wamekuhamisha. Hivyo, mtu aliyetwaliwa na Succubus au Incubus anatakiwa kuhamishwa na wachungaji wenye uwezo wa kukemea mapepo.

Katika njia ya tano, pepo likisikia unataka kwenda kwa mchungaji ili liachane na wewe litajenga uadui na wewe. Litajenga uadui mkubwa! Ukienda lazima wachungaji wafanye maombi makali kuweza kulitenganisha na wewe, na kuhakikisha halitarudi tena kwako kwa namna yoyote ile.

Incubus wanapenda nywele! Wanasemekana kuwanyemelea sana wanawake wenye nywele za rangi ya shaba au rangi ya kimanjano! Inasemekana hutumia muda mwingi kushangaa nywele kuliko kufanya mapenzi na mwanamke. Kwa hiyo nywele nzuri, hasa za shaba au kimanjano, ni faida kwa mwanamke; lakini wale waliotwaliwa na Incubus wanatakiwa maombi.

Mtu kufanana na mtu mwingine inaweza kuwa ni kwa sababu ya muingiliano wa vinasaba vya mababu zetu (‘ancestral DNA’) lakini Succubus na Incubus ni namna nyingine ambapo mtu anaweza kufanana sana na mtu mwingine. Aidha, inawezekana kabisa kwamba kila mtu ana pacha wake sehemu fulani duniani (kutokana na mapenzi ya Mungu).

No comments:

Post a Comment

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...