Monday, 27 November 2017

AKILI INAYOMTEGEMEA MUNGU INA NGUVU KUBWA KULIKO ULIMWENGU WOTE

253. Tunapofunga na kumwomba Mungu hakuna malaika, mwema au mbaya, mwenye nguvu kuliko akili ya mwanadamu. Kwani kama uweza ni kitu cha thamani zaidi katika ulimwengu huu; hivyo, akili inayomtegemea Mungu ina nguvu kubwa kuliko ulimwengu wote. Kwa hiyo akili ya namna hiyo inaweza kutengua uchawi, inaweza kutengua kazi zote za kishetani.

Hakuna dawa ya uchawi hapa duniani. Kuna dawa ya madhara yanayosababishwa na uchawi. Kwa hiyo dawa halisi ya uchawi si kwenda kwa mganga wa kienyeji, au mchawi mwingine kutafuta tiba, au kwenda kanisani au msikitini kufanyiwa maombi, ni kuwa karibu na Mungu akilini mwako. Akili, iliyo karibu na Mungu, ina nguvu kubwa kuliko vyote ulimwenguni.

1 comment:

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...