Bissau, mji maarufu katika bara la Afrika, kitovu kikuu cha biashara ya madawa ya kulevya katika bara la Ulaya, makao makuu ya CS-Bissau.
CS-Bissau, Tawi la Kolonia Santita la Ginebisau na nchi zote za Afrika ya Magharibi na Kaskazini isipokuwa Moroko ambayo iko katika kanda ya Ulaya, inaongozwa na jambazi sugu wa Ginebisau Aregado Midana. Midana ana umri wa miaka 51. Alizaliwa Jumapili ya tarehe 8/3/1941. Ana wake watatu, watoto tisa na wajukuu wawili.
Aregado Midana alikamatwa na kufungwa maisha nchini Ginebisau mwaka 1993, baada ya operesheni ya kung’oa mizizi ya Kolonia Santita duniani kote kukamilika.
No comments:
Post a Comment