Shetani anaweza kukudanganya kwa kukuambia ombeni bila kukoma, wewe ukakesha kuomba na kesho ukaendesha gari lako kuelekea kazini ambako una kikao cha muhimu hali kadhalika. Ukifika kazini unasinzia kwenye kikao unaonekana teja, kumbe ni kazi ya Ibilisi. Tujifunze namna ya kuzipima roho, si kila roho inatoka kwa Mungu.
Shetani ana mbinu nyingi za kuwateka wana wa Mungu. Mwanzo sura ya tatu inaonyesha jinsi Hawa alivyoona tunda linang’aa na akazama kwenye tunda pasipokujua kuna mauti ndani yake. Shetani anaangalia kipengele unachokitumia kuchukua maamuzi magumu naye anavaa jezi kama ya kwako ili usimgundue. Roho Mtakatifu akiwa anakuongoza, penye hila nafsi yako itakuongoza.
Kuwa makini na manabii wa uongo.
ReplyDelete