Sunday, 24 September 2017

Boti Katika Bahari ya Baltiki

Boti ya kahawia ya mvuvi wa Kideni iliyotumiwa na Frederik Mogens na Radia Hosni kuwafuatilia majambazi wa Kolonia Santita, waliokuwa wamemteka nyara Daniel Yehuda, kuanzia Kangelunden mpaka Dragør mpaka Saltholm, kilometa nne au tano kutoka Copenhagen.

Bila boti ya mvuvi wa Kideni katika Bahari ya Baltiki aliyekuwa akitoka katika safari zake za uvuvi siku ile usiku, Mpelelezi wa Tume ya Dunia Daniel Yehuda angeuwawa kinyama katika kisiwa cha Saltholm. Si yeye tu. Hata Radia Hosni angeuwawa kinyama, baadaye, katika hoteli ya D’Angleterre.

Vijana wa Tume, Radia Hosni na Frederik Mogens, walipotoka katika Msitu wa Mfalme wa Kangelunden, huku wakipigwa sana na baridi, waliondoka na boti mpaka Saltholm (katikati ya Swideni na Denmaki katika Ukanda wa Bahari wa Øresund) ambapo Mungu aliwasaidia wakamwokoa mwenzao. Kwa sababu hiyo, kwa sababu ya wokovu huo, Radia Hosni aliokolewa pia.

No comments:

Post a Comment

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...