Tuesday, 26 September 2017

Maabara ya Methi

Maabara ya kutengenezea madawa hatari ya kulevya kuliko yote duniani yaitwayo methamfetamini au hielo. Mwaka 2013 wale wanawake wawili wa Kitanzania waliokamatwa nchini Afrika Kusini kwa tuhuma za kusafirisha methamfetamini, hawakuwa na methamfetamini, walikuwa na dawa inayotumika kutengeneza methamfetamini.

Methamfetamini (methi) huweza kutengenezwa nyumbani. Mbolea ya amonia (‘ammonium fertilizer’ ), na lithi (‘lithium’), kutoka ndani ya betri za kawaida kwa mfano, huwekwa ndani ya chupa ya kawaida ya soda na kuifunika. Kemikali zinapofanya kazi hutoa si tu methi, lakini pia fukizo (‘fumes’); lakini ambazo zina uwezo wa kulipuka.

Hielo ni tofauti na kokeini kwa sababu inaunguza. Humfanya mtumiaji ajisikie raha ya kupindukia, nguvu, na makini! Mtumiaji huweza kukaa kwa saa ishirini na nne kwa siku bila lepe la usingizi, anaweza kufanya kazi kwa wiki nzima au wiki mbili bila kupumzika.

Methi huvutwa kwa kutumia buruma (‘pipe’) inayomlewesha mtumiaji kwa haraka na vizuri zaidi.

Matokeo mabaya ya baadaye ya utumiaji wa madawa haya ya ajabu ni pamoja na matatizo makubwa ya afya ya akili, na ukosefu kabisa wa hamu ya kula na kulala. Unaweza kujisikia kama vile unataka kuurarua uso wako wote! Kujikinga na dalili za namna hiyo, waathirika hulazimika kuvuta hielo zaidi.

Kukosa usingizi ni kubaya. Ukizidi kukaa kwa muda mrefu bila kulala, mwishowe utaugua ugonjwa unaitwa ‘matatizo ya akili ya wasiwasi’ (‘severe paranoid psychosis’).

Kama shumuya (heroini), ukitumia hielo utajisikia raha ya kupindukia. Raha unayoipata kwa kukuvuta hielo ni zaidi ya asilimia 1200 ya raha unayoipata kwa kuvuta bangi, heroini na kokeini kwa pamoja.

Kwa kawaida watu huanza kuvuta hielo baada tu ya saa sita za usiku, muda ambao watu wengi wamelala. Ukishavuta, au kujidunga, utataka buruma nyingine, utataka tena kujidunga. Kisha utafanya mambo ya ajabu kama kusafisha nyumba hadi asubuhi.

Dozi kubwa ya hielo huweza kusababisha kiharusi, maruweruwe, ugonjwa wa moyo, na hata kifo.

Soma zaidi hapa: http://bit.ly/methamfetamini

No comments:

Post a Comment

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...