Monday, 4 September 2017

Daudi wa Mapandikizi ya Dhambi

241. Ondoa pandikizi la dhambi liitwalo unafiki, kuwa au kumpata Musa, katika maisha yako.

Kilele cha mafanikio ya kila mtu ni Kanaani aliyotayarishiwa na Mwenyezi Mungu katika maisha yake. Katika maisha yetu kuna Farao na Musa. Farao ni rafiki wa uongo, Musa ni rafiki wa kweli. Farao na Musa hawaji katika maisha yetu kwa kubahatisha. Wameteuliwa na Mungu ili watusaidie kufika Kanaani, katika nchi zetu za ahadi, tukiwa tumekomaa na kukamilika.

Ukiondoa dhambi ya unafiki utakuwa Musa kwa ajili ya mtu mwingine, na mtu mwingine atakuwa Musa kwa ajili yako, kwa jina la Yesu Kristo.

Ubatizo ni toba iletayo ondoleo la dhambi. Mwangushe Goliati wa unafiki katika maisha yako kwa kumtumia Yesu Kristo, ambaye ni Daudi wa mapandikizi yote ya dhambi katika maisha yetu.

No comments:

Post a Comment

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...