Monday 17 July 2017

Mungu ni Mkuu

234. Mungu ni mkuu na ana haki ya kufanya lolote analotaka kufanya. Huu utakuwa ni udhalimu isipokuwa kwa ukweli mmoja tu kwamba kila jambo analofanya Mungu hata liwe baya au zuri au kubwa au dogo kiasi gani, limehamasishwa na upendo mkuu na wa ajabu sana ndani yake. Hata majaribu yetu ni matendo makuu ya upendo, kama ilivyokuwa kwa Ayubu au kama inavyooneshwa katika Waebrania 12:5-11. Kwa sababu ya upendo alionao kwetu Mungu ataruhusu majaribu yatupate, kwa sababu bila majaribu hayo hatutakamilika kama anavyotaka tukamilike.

Tulipokuwa watoto tuliadabishwa na wazazi wetu; mara ngapi tumewashukuru wazazi wetu kwa upendo waliotuonyesha? Kama wazazi, tumewaadabisha watoto wetu; mara ngapi wametushukuru kwa adhabu tulizowapa? Inawezekana kabisa kuwa hawajawahi kutushukuru, lakini adhabu tunazowapa zinalenga waishi katika maadili tunayotaka waishi; na inawezekana kabisa kuwa hatujawahi kuwashukuru wazazi wetu, lakini adhabu walizotupa zililenga tuishi katika maadili waliyotaka tuishi.

Tunawaadhibu watoto wetu kutokana na upendo au chuki? Bila shaka tunawaadhibu kutokana na upendo. Hivyo kwa nini wasitushukuru kwa adhabu tunazowapa? Kwa sababu kwa sasa hawawezi kuona au kuamini ni kiasi gani tunawapenda, lakini baadaye wataona na wataamini.

Kwa watoto au vijana ambao bado hawajakomaa ni sifa bainifu kwao kutokuona picha kubwa ya mambo ya mbeleni, isipokuwa ile tu iliyoko moja kwa moja mbele yao kwa wakati huo. Katika nyakati za majaribu sisi si watoto, kwa maana ya kiroho.

No comments:

Post a Comment

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...