235. Dhambi ni dhambi ni dhambi.
Dhambi hata iwe kubwa au ndogo kiasi gani zote ni dhambi na kila mtu ana dhambi. Dhambi ya kuua mtu haiwezi kuwa sawa na dhambi ya kuiba simu lakini zote ni dhambi. Hivyo kama zote ni dhambi na kila mtu ana dhambi hupaswi kumhukumu mtu unayedhani au unayejua ana dhambi.
Kuua mwizi mathalani ni dhambi na ni kosa kisheria ni sawa na mauaji mengine yoyote yale. Damu ya huyo uliyemuua itakusumbua sana maishani mwako, hata kama huyo uliyemuua ulimuua kwa makusudi au kwa bahati mbaya, hata kama huyo uliyemuua alikuwa mwizi. Kama ni mwizi acha vyombo vya dola vishughulike naye kwani yeye ana dhambi na wewe una dhambi pia.

Kuhukumu ni kazi ya Mungu.
ReplyDelete