Monday 5 June 2017

Kupambana na Mungu

228. Mtu anayejaribu kupambana na Mungu anajaribu kupambana na jambo lisilowezekana. Hatakuwa na uwezo wa kushinda. Kufanya hivyo ni upumbavu usioweza kuelezeka, lakini wanadamu hatukomi kufanya hivyo.

Kinachotokea katika dunia hii si kitu kizuri cha kuzoea au hata kufikiria. Hivyo tuna haki ya kuwa na mawazo, hasira na wanyonge kuhusiana na suala zima la maisha yetu hapa duniani. Hata hivyo hali hii itabaki kuwa hivyo kwa sababu Mungu ametaka iwe hivyo kwa sasa. Kwa maana hiyo, hekima ni kukubaliana na mapenzi ya Mungu. Lazima tukubaliane na kisichoweza kufikirika kuweza kubadilika.

Watu wote ni wa Mungu, watu ni matatizo. Wewe huna mtu, lakini bado unapambana na Mungu kuhusu watu.

Matatizo tunayopitia si matatizo kwa ukuaji wetu. Mungu hafanyi hivyo eti kutukomoa. Anafanya hivyo kwa faida yetu ya baadaye.

1 comment:

  1. Kinachosababisha tupambane na Mungu ni matatizo, ambayo huletwa na watu, na tunapambana kwa silaha ya uongo.

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...