Kusudi mimba itungwe lazima kuwepo na kromosomu X na kromosomu Y.
Kromosomu ni nyuzinyuzi katika kiini cha seli zenye jeni au DNA, ambazo
hubeba taarifa kuhusu sifa za kimaumbile zinazorithishwa kwa kiumbe hai
kutoka kwa mama na baba wa kiumbe hicho. Kwa upande wa Yesu Kristo,
katika hali ya kawaida, kromosomu X ilitoka kwa Maria Magdalena na
kromosomu Y ilitoka kwa malaika Gabrieli. Yesu alikuwa Myahudi lakini
Kristo ni Mungu. Yesu Kristo alikuwa binadamu kama sisi, lakini alikuwa
na utukufu na alikuwa na damu ya Mungu iliyotakasika. Damu kama hiyo
ndiyo inayotiririka katika miili ya kila mmojawetu ijapokuwa ni damu ya
Adamu, ambayo bado haijatakaswa.
Damu ya Yesu si kitu kidogo.
Ilipomwagika msalabani ilifunika dunia nzima. Ndiyo maana tukasamehewa.
Bila damu hiyo, bila utukufu huo wa Mungu, hakuna binadamu
atakayeokolewa, hakuna pepo atakayeondolewa.
Mungu ni mtakatifu
na kwa maana hiyo hatendi dhambi. Hivyo, hauwi wala hatesi. Tunajiua na
kujitesa wenyewe. Ametupa hiari ya kuchagua mema au mabaya. Lakini
anamtumia Shetani kama wakala wake wa kutoa adhabu kwa binadamu pale
tunapoenenda sawasawa na machukizo yake.
Damu ina nguvu kuliko
Shetani na ina nguvu kuliko kuzimu. Unapojifunika kwa damu ya
Mwanakondoo, Shetani hataweza kukuona. Hivyo, hataweza kukudhuru. Lakini
usipojifunika kwa damu ya Mwanakondoo, Shetani atakuona. Hivyo,
atakudhuru. Atakudhuru kwa sababu Mungu atakuwa ameruhusu akudhuru, kwa
sababu ya uhuru wa kuchagua mema au mabaya aliotupatia, ijapokuwa ana
uwezo wa kuzuia asikudhuru. Kwa mtindo huo Mungu anakuwa ametoa adhabu
kwa binadamu.
Shetani naye anamtumia Mungu kama wakala wake wa
kutoa adhabu kwa binadamu kwa sababu Shetani siku hizi anaishi
makanisani na misikitini. Anamtumia Mungu kwa maana ya kutuingiza
dhambini huku tunaona, tukiwa mbele ya uwepo wa Mungu tunayemwabudu.
Mungu anaishi ndani ya damu, maisha ya Mungu yalikuwa yanaishi ndani ya
mwili wa Yesu Kristo, anaishi ndani ya miili yetu. Unapokula damu,
unapokunywa damu, unakula, unakunywa sehemu ya Mungu aliyekuumba.
Shetani anapenda damu kumdhihaki Mungu kwa sababu Mungu anapenda damu
na bila damu hakuna binadamu atakayeokolewa. (Bila damu wokovu hauna
maana). Usimwogope Shetani eti kwa sababu anapenda damu, mwogope Mungu
kwa sababu ndiye anayejua umuhimu wa damu hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Roho Yako
289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...
-
Mercury Cougar ya John Murphy aliyonunua mwaka 1990 kwa gharama kubwa huko Michigan nchini Marekani. Gari hilo lililorekebishwa kwa ajili ...
-
Siku ya kuzaliwa ni siku ya kwanza ya safari nyingine ya siku 365, saa 5, dakika 48, sekunde 46 na maili milioni 600 kulizunguka jua. Safi...
-
KITENDAWILI CHA KOLONIA SANTITA Shilingi milioni moja za Kitanzania kushindaniwa ndani ya miezi sita kuanzia leo Swali: Kila namba ...
No comments:
Post a Comment