224. Watoto wadogo wanakufa. Watu wazima wasiokuwa na hatia wanakufa vitani na katika majanga mengine ya asili. Kwa nini? Watoto wadogo wanaokufa walikuja duniani kufanya nini? Kwa nini watu wasiokuwa na hatia wanakufa ilhali Mungu yupo na asiwaepushe na matatizo ya dunia hii? Kama aliweza kuzuia binadamu wasiishi majini kwa sababu watakufa kwa nini asizuie matatizo yasiwapate watoto na watu wazima wasiokuwa na hatia? Sisi ni wadogo sana na Mungu ni mkubwa mno. Jibu hatutaweza kulielewa pamoja na kwamba tumepewa. Hata hivyo, Mungu hababaishwi na mwili. Anababaishwa na roho.
Adamu na Hawa walipotenda dhambi waligundua kuwa kumbe walikuwa na miili, walipogundua kuwa walikuwa uchi, kisha Mungu akawalaani. Miili yao ikakosa thamani mbele ya Mungu, sisi wote tukalaaniwa pamoja nao. Kwa Mungu hii miili haina thamani hata kidogo. Chenye thamani ni roho.
Mungu angekuwa anababaishwa na mwili asingeruhusu Shetani autese mwili wa Ayubu kiasi chote kile isipokuwa roho yake, wala tusingekuwa tunateseka, wala watoto wadogo wasingekuwa wanakufa, wala watu wasiokuwa na hatia wasingekuwa wanakufa vitani au katika majanga mengine yoyote yale katika dunia hii.
Lakini jibu lipo, katika kitabu cha Ayubu 40:1-24, lakini hakuna atakayelielewa.
Mungu anayezungumzwa ni Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo, Anayeruhusu maovu yatendeke kwa sababu ya dhambi mbili za asili: Kiburi na Zinaa. Kiburi ni dhambi ya Ibilisi. Zinaa ni dhambi ya wazazi wetu wa kwanza. Hivyo, kila kinachofanyika kimo ndani ya mpango mkuu wa Mungu wa ukombozi wa dunia hii.
Kwa watoto waliofariki juzi kwa ajali mbaya ya barabarani huko Karatu mkoani Arusha pamoja na dereva na walimu wao: Bwana alitoa, na Bwana ametwaa; jina la Bwana libarikiwe.
ReplyDelete