Thursday, 11 May 2017

Magdalena Carmen Frieda Kahlo y Calderón

Frida Kahlo de Rivera, Magdalena Carmen Frieda Kahlo y Calderón, mwanamke aliyebadilisha maisha yake kwa kujichora mwenyewe, mwenye asili ya India kwa upande wa mama yake na Ujerumani kwa upande wa baba yake, mchoraji wa kike maarufu kuliko wote nchini Meksiko, alikuwa shujaa wa maisha ya Mtoto wa Rais wa Meksiko Debbie Patrocinio Abrego.

John Murphy alipoingia katika chumba cha kifahari cha Debbie Patrocinio Abrego huko Los Pinos nchini Meksiko, alishangazwa na picha kubwa tatu ukutani nyuma ya kitanda cha Energy Opus: wanawake wawili mwanamume mmoja, waliyoonekana kuwa wa muhimu sana katika maisha ya Debbie.

Mwanamume alikuwa Marciano Moreno Herrera, mchumba wa Debbie aliyeuwawa kwa amri ya Panthera Tigrisi. Wanawake walikuwa Wanda Castellanos, rafiki mpenzi wa Debbie, mtoto wa Panthera Tigrisi; na Frida Kahlo, shujaa wa maisha ya Debbie, aliyezaliwa Coyoacán na kufia Coyoacán jijini Mexico City.

“Huyo wa kushoto ni shujaa wa maisha yangu. Frida Kahlo. Hiyo michoro mitatu unayoiona hapo ukutani ni miongoni mwa kazi zake maridadi. Maarufu dunia nzima. Alizaliwa Coyoacán na kufia Coyoacán. Ndiyo maana Coyoacán ni sawa na Maka kwangu; tumenunua hata ‘managerie’ hapo, shamba la wanyama wa mwitu.

Huyo wa katikati ni Marciano. Hapo ni miaka kumi iliyopita. Alikuwa bado mdogo, miaka kumi na tisa. Aliipiga katika sherehe yangu ya ‘quinceañera’ ya kutimiza miaka kumi na tano, kipindi hicho tukiwa bado tunaishi La Soledad, Canatlan, Durango; halafu akaniletea kama zawadi baada ya kuisafisha katika studio ya mji wa nyumbani kwao Ciénega de Caballos.

Huyo wa kulia ni rafiki yangu. Wanda Castellanos. Lakini kuanzia Jumanne iliyopita si rafiki yangu tena.” – Debbie Patrocinio Abrego

No comments:

Post a Comment

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...