Thursday, 23 March 2017

Renault Safrane

Gari la kifahari la mpelelezi wa Tume ya Dunia kutoka Denmaki Frederik Mogens Schaldemose Friis Brodersen (Frederik Mogens), Renault Safrane, lililotumika kuwabeba Vijana wa Tume jijini Copenhagen katika harakati za Operation DC (Operation Devil Cross), lililokuwa na namba za usajili za kijematria.

Renault Safrane ya Frederik Mogens ndiyo iliyotumika kumpokea John Murphy na Daniel Yehuda katika Uwanja wa Ndege wa Copenhagen Kastrup, na ndiyo iliyotumiwa na Daniel Yehuda kwenda na kurudi Frederiksberg (nje ya Copenhagen) kuchunguza kwa mara ya mwisho Makao Makuu ya CS-Copenhagen (Tawi la Kolonia Santita Skandinavia), kabla ya kutekeleza Operation Kimbunga ya Operation Devil Cross.

Gari la Mogens lilikuwa na uwezo wa kubadilika rangi kati ya nyeusi na kijivu kwa sababu za kiusalama. Namba zake za usajili zilikuwa haziwezi kusomwa na kompyuta za polisi wa Copenhagen, na zilikuwa na uwezo wa kubadilika na kuwa namba yoyote ambayo Mogens angetaka.

Katika kompyuta za magari ya polisi wa Copenhagen namba za usajili za magari ya Mogens zilisomeka ‘Blocked’, kama zilivyo namba za usajili za magari mengi ya kifalme na machache ya kiserikali ya Denmaki.

Renault Safrane ya Mogens halikuwa gari la kawaida. Lilikuwa na namba za kiroho za kijematria. Yaani 2484. 2484 maana yake ni Frederik Mogens Schaldemose Friis Brodersen. Wakati James Bond hujulikana kama 007, Frederik Mogens hujulikana kama 2484, kwa sababu zilizoko nje ya uwezo wetu.


No comments:

Post a Comment

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...