Saturday, 25 February 2017

The Silent Predator of the Deep

Nyambizi ya Panthera Tigrisi iitwayo SPD (‘the Silent Predator of the Deep’) ikiyoyoma katika Ghuba ya Meksiko; baada ya Panthera Tigrisi kutangaza vita na Serikali ya Meksiko Septemba 16, 1986, ‘The People’s Don’ akiwa na makomandoo wake Narochnitskaya Belinsky na Nicolas Kahima Kankiriho (‘Kahima the Warrior’) na wanajeshi wengine 17 wa ‘Autodefensa’!

Nyambizi ya Panthera Tigrisi ilikuwa na teknolojia ya kisasa kabisa kwa kipindi hicho (‘Stealth technology’ au ‘LO technology’) iliyokuwa ikifanya isigundulike kirahisi mara tu baada ya kuzama yote majini. Ilikuwa haina sauti, hivyo kufanya meli au boti au nyambizi za vyombo vya dola na maadui zake kushindwa kubaini kirahisi mahali ilipokuwa. Ndiyo maana ikaitwa ‘the Silent Predator of the Deep’.

Teknolojia ya ‘Stealth’ au ‘LO’ (‘Low Observable’) si teknolojia ya kawaida. SPD ilikuwa na uwezo wa kuzama hadi kina cha meta 150 na kubakia huko kwa miezi mitatu, bila kuwa na haja ya kuibuka tena.

1 comment:

  1. ‘Stealth technology’ huondoa sauti kwenye injini na kwenye propela linaloendesha nyambizi. Mawimbi ya sauti yanayotoka kwenye injini na kwenye propela hayafiki mbali kiasi cha mawimbi hayo kuweza kunaswa na teknolojia za vyombo vya dola au vyombo vya maadui.

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...