Spishi ya miti kama mfune inayopatikana katika bara la Amerika ya Kaskazini iitwayo ‘Fagus Grandifolia’ au ‘American Beech’, Kiongozi wa Kanda ya Amerika ya Kaskazini ya Tume ya Dunia Kamishna Profesa Randall Buchanan Ortega alipoegemea huko Boston nchini Marekani; Dereva wa Tume Wayne Serrano alipompa tiketi ya ndege ya shirika la ndege la Uingereza (BA) ya kwenda Copenhagen, kuhudhuria kikao cha dharura cha Tume ya Dunia.
Kwa sababu za kijiografia, katika majira ya baridi, kisaa, Copenhagen haina tofauti na Tunis, Tunisia na London, Uingereza. Iko mbele kwa saa sita kuilinganisha na Boston, Massachusetts, Marekani; na La Paz, Bolivia, Amerika ya Kusini. Iko nyuma kwa saa mbili kuilinganisha na Dar es Salaam, Tanzania; na nyuma kwa saa tano na nusu kuilinganisha na Yangon (Rangoon), Myama (Bama), Kusini-mashariki mwa bara la Asia. Faksi ya Oslo ilifika katika ofisi za Kanda ya Amerika ya Kaskazini ya Tume ya Dunia jijini Boston asubuhi ya Jumatano (Jumatano hiyohiyo ilipotumwa) wakati kamishna akiwa Burlington katika mojawapo ya kliniki zake za madawa ya kulevya. Kamishna, alivyorudi ofisini mchana, alipewa taarifa za faksi na maelekezo yote ya safari yake ya Copenhagen; hivyo akaenda nyumbani kwa ajili ya maandalizi ya safari, lakini akatumia muda mwingi nje ya nyumba katika mti wa ‘Fagus Grandifolia’; ambapo mawazo yalimsonga na kupitiwa na usingizi. Dereva wa Tume Wayne Serrano alipofika kuleta tiketi ya ndege kamishna alijiandaa; kisha Serrano akamwendesha mpaka uwanja wa ndege wa Logan, ambapo Ortega alisafiri kuelekea Copenhagen nchini Denmaki.
Kiongozi wa Kanda ya Amerika ya Kaskazini ya Tume ya Dunia na Mshauri wa Madawa wa Gavana wa Massachusetts, Kamishna Profesa Randall Buchanan Ortega wa Boston nchini Marekani, alikuwa mstari wa mbele katika vita kati ya Kolonia Santita na Tume ya Dunia. Kamishna ni mtu aliyewahi kukumbana na matatizo mengi katika operesheni za tume, hivyo alikuwa na hofu kubwa alipopata faksi ya Oslo – iliyomtaka aondoke haraka kwenda Copenhagen kuonana na Kamishna Mkuu wa Tume ya Dunia.
Makamishna wote wa Tume ya Dunia wana haki ya kuwa na hofu pindi wanapokabiliana na miito ya kiusalama ya Oslo, wote walishapata matatizo katika juhudi zao za kutetea afya na amani ya dunia.
No comments:
Post a Comment