206.
 Kutoka nyumbani kwako hadi kazini kwako na kutoka kazini kwako hadi 
nyumbani kwako, umeepuka wastani wa mitego 10,000 ya Shetani! Kuwa na 
huruma kwa malaika anayekulinda. 
Mungu
 ana uwezo wa kukuwekea ulinzi kulia na kushoto yaani anayekulinda naye 
ana mlinzi wake. Lakini wakati mwingine anaacha ufuate kile ambacho moyo
 wako unataka kwa sababu hataki kukulazimisha ijapokuwa uwezo huo anao. 
Mungu hakukuumba kuwa roboti. Alikuumba kuwa huru kuchagua mema au 
mabaya usije ukamlaumu baadaye kwamba ulimchagua yeye kwa sababu hukuwa 
na uhuru. Msikilize Roho wa Mungu, kabla na katika kila jambo 
unalofanya. 
Ndugu
 zangu, malaika wanatulinda. Wako katikati ya maadui zetu na sisi. 
Hatujui ni mara ngapi malaika wameingilia kati kuokoa maisha yetu, 
kutuepusha na nguvu za Shetani na malaika wake wakorofi. Lakini nina 
hakika ya kwamba wamefanya hivyo mara nyingi katika mazingira ambapo 
aghalabu sisi huwa hatuelewi. 
Mungu
 anataka tujifunike kwa ngao yake. Yaani, tuwe na imani iliyokomaa 
katika Bwana na yeye atatufunika. Maana ya kauli hiyo ni kwamba kila 
kiungo cha miili yetu kuanzia unyayo hadi kichwa lazima kifunikwe kwa 
silaha ya Mungu, ambayo Mungu anaiita panoplia. Panoplia haimo katika 
kamusi ya Kiswahili au Kiingereza, lakini maana yake ni ‘ngao kamili ya 
Mungu’. Hii si tu silaha ya Mungu. Ni silaha kamili ya Mungu 
tunayotakiwa kujifunika kwayo. 
Sasa
 litambua hili: ushindi ni lazima kwa sababu Daudi wetu Yesu Kristo 
ameshamshinda Goliati wao Shetani. Amemshinda ili aishi ndani yetu na 
anaishi ndani yetu. Lakini hatutaweza kumshinda Shetani na malaika wake 
mpaka tutambue kuwa wapo na tuamini kuwa Mungu atawashinda kama tutampa 
nafasi ya kufanya hivyo kwa kuwa watiifu kwake. 
Kuwa
 na huruma kwa malaika anayekulinda ni kujifunika kwa silaha kamili ya 
Mungu. Ukijifunika kwa panoplia utamrahisishia kazi malaika wako, 
aliyepewa jukumu na Mwenyezi Mungu kukulinda. 

Mungu anataka tuwe na upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, na kiasi katika mambo tunayoyafanya. Lakini sifa hizi hazitapatikana hadi tumtii Mungu kupitia Roho Mtakatifu.
ReplyDelete