Bastola
 ya majambazi wa Kolonia Santita iitwayo Akdal Ghost kutoka Uturuki, 
yenye uwezo wa kubeba kwa wakati mmoja risasi kumi na tano katika chemba
 yake, iliyokamatwa na Polisi wa Tume ya Dunia huko Varsovia nchini 
Meksiko. 
Akdal
 Ghost ni bastola iliyokuwa imetengwa kuwaua Vijana wa Tume John Murphy 
na Frederik Mogens lakini wakasaidiwa na Mtoto wa Rais Debbie Patrocinio
 Abrego na walinzi wake. Hata hivyo majambazi waliokuwa wametumwa 
kufanya kazi hiyo walikamatwa kabla hawajatekeleza jukumu lao, na 
kupelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Tume ya Dunia cha Zona Rosa 
kwa ajili ya mashtaka. Lakini hawakushtakiwa. Walipewa msamaha, wa 
Programu ya Ushahidi ya Tume ya Dunia (‘WODEA Witness Protection 
Programme’) kwa makubaliano ya ushirikiano wa asilimia 100 katika kesi 
dhidi ya makamanda wa Kolonia Santita. 
WWPP
 (‘WODEA Witness Protection Programme’) ni Programu Maalumu ya Ushahidi 
ya Tume ya Dunia ya kuwakinga mashahidi wa kihalifu kwa kuwapa makazi 
mapya, majina mapya, kazi mpya, historia mpya ya maisha, na sura mpya, 
kuwakinga na Sheria ya Kitalifa ya Kolonia Santita. Ukivunja Sheria ya 
Kitalifa ya Kiapo cha Swastika cha Kolonia Santita utauwawa, tena 
utauwawa kinyama, wewe na familia yako. 
Kitalifa
 ni utiifu kamili, woga, umbali (kwa maana ya kuwa mbali na biashara ya 
mamafia wengine mpaka kwa makubaliano maalumu) na nidhamu ya 
kutoshirikiana na mamlaka zote za serikali. Ukishtakiwa kwa kosa la 
madawa au ujambazi ambalo hukufanya, utatumikia kifungo mpaka mwisho 
bila kushirikiana na polisi (kwa maana ya kutaja aliyehusika au 
waliohusika na uhalifu huo) hata kama aliyehusika au waliohusika hana au
 hawana uhusiano wowote na Kolonia Santita. Falsafa ya Kitalifa ni 
Sheria ya Kitalifa ya Kiapo cha Swastika cha Kolonia Santita. Adhabu ya 
kuvunja sheria hiyo ni kifo. 

No comments:
Post a Comment