Kiswahili ni lugha ya Kibantu na lugha kuu ya kimataifa ya biashara
ya Afrika ya Mashariki ambayo; maneno yake mengi yamepokewa kutoka
katika lugha za Kiarabu, Kireno, Kiingereza, Kihindi, Kijerumani na
Kifaransa, kutoka kwa wakoloni waliyoitawala pwani ya Afrika ya
Mashariki katika kipindi cha karne tano zilizopita.
Lugha ya
Kiswahili ilitokana na lugha za Kisabaki za Afrika Mashariki; ambazo
nazo zilitokana na Lugha za Kibantu za Pwani ya Kaskazini Mashariki za
Tanzania na Kenya, zilizotokana na lugha zaidi ya 500 za Kibantu za
Afrika ya Kusini na Kati.
Lugha za Kibantu zilitokana na lugha za
Kibantoidi, ambazo ni lugha zenye asili ya Kibantu za kusini mwa eneo
la Wabantu, zilizotokana na jamii ya lugha za Kikongo na Kibenue – tawi
kubwa kuliko yote ya familia ya lugha za Kikongo na Kinijeri katika bara
la Afrika. Familia ya lugha za Kikongo na Kibenue ilitokana na jamii ya
lugha za Kiatlantiki na Kikongo; zilizotokana na familia ya lugha za
Kikongo na Kinijeri, ambayo ni familia kubwa ya lugha kuliko zote
duniani kwa maana ya lugha za kikabila.
Familia ya lugha ya
Kiswahili imekuwepo kwa karne nyingi. Tujifunze kuzipenda na kuzitetea
lugha zetu kwa faida ya vizazi vijavyo.
Assembly wants Kiswahili adopted as one of the official languages of the Community
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Roho Yako
289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...

-
Uwanja wa Ndege wa Copenhagen-Roskilde: uliotumiwa na Tume ya Dunia na Kolonia Santita kwa pamoja – kilometa tisa kutoka katika Kanisa ...
-
Mpelelezi wa Tume ya Dunia kutoka Jerusalem, Israeli, Kanali Daniel ‘Yehuda Ben-Asher’ Ebenezer, Daniel Yehuda, alikuwa komandoo wa kit...
No comments:
Post a Comment